Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa amesema  sasa amechoka kusikia mauaji kwenye mikutano ya kisiasa ya CDM na  atatumia rungu lake kufutia usajili chama chochote kitakachoshindwa  kutunza amani ya nchi.Tendwa amewaambia waandishi wa habari hatishiki na  chama chochote kuwa na wabunge kwani sheria inamruhusu kufuta chama  hata kama kina wabunge 100.
Katika hali ya kushangaza Tendwa ameshauri vyama visubiri nyakati za uchaguzi ndipo vifanye mikutano ya kisiasa.Hata hivyo amekiri sheria inaruhusu vyama kufanya mikutano na maandamano wakati wowote.
Source:Habari Radio Tumaini.