Subscribe:

search

.

Thursday, 9 August 2012

KIJANA ALIYEUAWA KWA TUHUMA ZA KUIBA KOKI YA BOMBA JIJINI MWANZA







Ni ukatili gani huu...?








Mwili wa marehemu.



Wananchi wa maeneo hayo wakiangali huku wakijiuliza maswali ya kwanini matukio ya kujichukulia sheria mikononi bado wanaendekezwa na Wananchi.


Koki aliyokutwa nayo marehemu Hassan Stanley.


Mwandishi wa habari Fabian Fanuel kutoka FPLUSS BLOG  akiwa na Mwandishi wa habari wa Kwaneema Fm Joshua Dede wakimhoji mwenyekiti wa mtaa wa Chanmwenda bi. Lucy Kapombe.


Mwenyekiti wa Mtaa wa Kiloleli bwana Joshua Josia Mnana akiwatoa maelezo mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na tukio la kifo cha Hassan Stanley.



Kaka yake Marehemu Hassan akimfunika kanga mdogo wake baada ya kukutwa na tukio la kuuawa kwake..


Mwili wa marehemu Hassan Stanley akiwa amefunikwa kanga na kaka yake.
Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Hassan Stanley asubuhi ya kuamkia leo majira ya saa kumi na moja  katika maeneo ya uwanja wa mbuzi Kiloleli jijini Mwanza, ameuawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa na kuchomwa moto hadi kupelekea mauti yake.

 Mwenyekiti wa mtaa wa maeneo tukio lilipotokea Bi Lucy Kapombe amesema kuwa haya ni matokeo na hasira walizokuwa nazo wananchi ambao wamekuwa wakilalamikia matukio ya wizi wa koki za maji maeneo mbalimbali katika jiji la Mwanza.

Amesema yeye binafsi hauingi mkono mwizi yeyote kuuawa bali wananchi wanatakiwa kuiacha sheria ifuate mkondo wake katika watuhumiwa wanaokuwa wamekamatwa kutokana na matukio mbalimbali ya uhalifu katika jamii yetu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Kiloleli b bwana Joshua Josia Mnana ameto wito kwa vijana wanohusika katika uhalifu mbalimbali kuacha ili wasije wakapatwa na matukio kwa hayo yaliyompata mwenzao.

Marehemu Hassana Stanley aliye na umari wa kati ya miaka 22 hadi 26 alikuwa mpiga debe katika kituo cha Kiloleli na ni kazi ambayo amekuwa akiifanya mpaka anakutwa na umauti.


Sote  tunalaani matukio ya wananchi kujichukulia sheria mikononi mwao.

CHANZO:-  fpluss.blogspot.com

0 comments: