Mwnyekiti wa
MISA-Tanzania Mohamed Tibanyendera, akizungumza na waandsihi wa habari kuhusu
hatua wanazozichukua dhidi ya Serikali kutokana na kulifungia gazeti la
MwanaHalisi.
---
Kamati ndogo iliyoundwa
na taasisi nne za kiraia nchini ambayo inaratibu kupigania haki ya kufunguliwa
kwa gazeti la MwanaHalisi, leo imeipa serikali siku saba kuliruhusu gazeti hilo
kuendelea kuchapishwa.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa kamati hiyo Marcossy Albanie, amesema hawana sababu yakwenda mahakamani juu ya jambo hilo kwasababu hata serikali haikutumia njia hiyo ya mahakamani kwani ilikuwepo badala yake wametumia sheria kandamizi ya vyombo vya habari inayopigiwa kelele na wadau wa habari.
Kamati hiyo inayoungwa mkono na taasisi tano za kiraia baadhi ya taasisi hizo ni MISA TANZANIA, TANZANIA HUMANRIGHTS DEFENDERS COALITIONS NA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU (LHRC) imeitaka serikalikutekeleza madai yafuatayo:-

- Kuitaka serikali kulifungulia gazeti la Mwanahalisi maramoja.
- Serikali badala ya kushughulikia Watetezi wa haki na wanahabari wanaofichua uovu ishughulike na wahalifu waluiomteka Dkt. Ulimboka.
- Serikali iache kabisa na ukandamizaji huu wa haki na uhuru wa habari.
WAANDISHI WA HABARI WAOMBWA YAFUATAYO SERIKALI ISIPOTEKELEZA HAYO:
- Kutochapisha habari yoyote itakayo wahusu Waziri wa Habari wa Wizara hiyo na Naibu wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo.
- Kusimama kidete kuunga mkono harakati hizo hadi zinapata ufumbuzi wake.
Chanzo:Audiface Jackson Blogspot.com
0 comments:
Post a Comment