Monday, 13 August 2012
TAKUKURU YAMTIA MAHAKAMANI ALIYEKUWA MHANDISI WA HALIMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA
Taasisi ya kuzui na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Mara imemfikisha Mahakamani Christopher Nyandiga aliyekuwa Mhandisi wa Halimashauri ya Wilaya ya Bunda ambaye kwa sasa amehamishiwa Wilaya ya Ludewa kwa makosa ya kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajili kinyume cha kifungu cha 22 cha Sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari,Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mara Yustina Chagaka ilisema kutokana na uganganyifu huo ameisababishia Serikali hasara ya jumla ya shilingi za Kitanzania milioni ishirini na nne (24,000,000) kinyume cha kifungu cha 10(1) cha jedwali la kwanza pamoja na vifungu vya 57(1) na 60(2) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi namba 200 iliyofanyiwa mapitio Mwaka 2002.
Alisema baada ya Uchunguzi uliofanywa na TAKUKURU ulibaini kampuni inayomilikiwa na mtuhumiwa huyo iitwayo MBULLY ENTERPRISES AND CIVIL WORK ilipewa zabuni na Halimashauri na Wilaya ya Bunda ya kuleta mashine ya windmill aina ya Poldaw ya mita 5.8 na mita 8.2 kwa gaharama ya shilingi milioni ishirini na nne kwa ajili ya mradi wa umwagiliaji mazao katika kijiji cha Kasuguti na kuleta vilivyo chakavu na visivyofaa kwa matumizi yaliyokusudiwa.
Taarifa hiyo iliieleza kuwa mtuhumiwa huyo pia aliwasilisha gharama ya shilingi milioni mbili(2,000,000) kwa ajili ya kuisimika na shilingi milioni (1,000,000,) yakuifanyia majaribio mashine hizo na kufanya jumla ya shilingi milioni ishirini na saba (27,000,000) kwa ajilki ya mradi huo.
Ushunguzi huo wa TAKUKURU ulibini mnamo Desemba 2007 mtuhumiwa huyo kwa niaba ya kampuni ya MBULLY ENTERPRISES AND CIVIL WEORKS aliwasilisha hati ya madai (invoice) nambari 0152 na (delivery Note) nambari 0252 kwa Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Bunda zenye maelezo ya uongo kwamba amenunua mashine mpya huku zikiwa ni chakavu na zisizofaa na kuisababishia Serikali hasara.
Kufuatia hali hiyo,Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mara Chagaka alitoa wito kwa Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za vitendo vya Rushwa wanapoona mazingira ya kufanyika.
Alisema kazi ya kupambana na vitendo vya Rushwa katika sehemu mbalimbali haifanywi na Taasisi hiyo pekee yake bali kila Mwananchi anapaswa kushiriki ili kuweza kukomesha vitendo hivyo kwa kuwa vinafifisha shughuli za kimaendeleo na kutopatikana huduma iliyo sahihi.
Chanzo:GSengo.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment