Al-Shabaab imejikuta katika ukingo wa kuvunjika baada ya kikundi hicho kuukimbia mji wa kimkakati wa Kismayo
mwishoni mwa mwezi wa Septemba kabla ya kufika kwa vikosi vya Jeshi la
Taifa la Somalia na Misheni ya Umoja wa Afrika huko Somalia (AMISOM)
Kikundi hicho chenye mafungamano na al-Qaeda kilipoteza Kismayo
wakati viongozi wake wa juu wakigombea madaraka, kujulikana na fedha, na
wapiganaji wa kikundi hicho wanakabiliwa na kupoteza morali, hususani
wale wanaohisi walistahili uongozi wa uandamizi wa kikundi hicho.
Kismayo ni mji mkuu wa mkoa wa tano ambao al-Shabaab imepoteza kwa miezi ya hivi karibuni baada ya Marka, Beledweyne, Baidoa na Hudur,
lakini Kismayo ulikuwa muhimu zaidi kwa sababu ulikuwa ngome kuu ya
kikundi hiki kwa miaka kadhaa na kutumika kama chanzo kikuu cha mapato.
Kupoteza huku haraka kwa maeneo kumesababisha kukosa utulivu mkubwa
ndani ya kikundi, kwani viongozi wake watashawishika kuendelea kujificha
kwa kuwa wanatafuta makazi mapya yenye usalama.
Sababu hizi, miongoni mwa nyingine, zinakigawanya kikundi hiki zaidi na kutengeneza kazi za chini chini kwa mvunjiko wake kamili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment