Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
Serikali
imetenga jumla ya shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kufikisha umeme katika
vijiji vya mikoa ya Lindi na Mtwara ikiwa ni mpango wa kufikisha
miundombinu ya umeme katika vijiji mbalimbali kwa asilimia therethini nchi
nzima ifikapo mwaka 2015.
Kaimu Meneja wa
Shirika la umeme TANESCO Mkoa wa Mtwara Mhandisi Daniel Kiando amewaambia
waandishi wa habari kuwa fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya miradi therathini
na moja (31) ambapo vijiji vilivyopo katika wilaya za Masasi, Newala na
Tandahimba vitanufaika.
“Mpaka sasa
tayari mradi umekamilika kwa asilimia mia moja katika kijiji cha Mbambakofi
kilichopo wilaya ya Tandahimba na wateja wanaendelea kujaza fomu kwa
ajili ya kuwekewa umeme katika nyumba zao,” amesema Kiando.
Kiando
amefafanua kuwa nyumba zitakazowekewa umeme ni zile ambazo zimeezekwa kwa bati
hivyo ametoa wito kwa wananchi kuezeka nyumba zao ili waweze kunufaika na mradi
huo pamoja na kurahisha maendeleo yao kwa ujumla.
Nae mkazi wa
kijiji hicho Asha Nalamba amesema kuwa amefurahishwa na kitendo cha Serikali
kupeleka mradi huo vijijini na tayari ameanza kujipanga kuezeka nyumba yake kwa
bati ili aweze kunufaika na umeme huo.
“Mimi nina
nyumba ya nyasi lakini tulivyotangaziwa mradi huu, nikaanza polepole kujipanga
na mpaka sasa nimeshanunua mabati ishirini, natarajia mwezi Novemba mwaka
huu kuzeeka,” amesema Nalamba.
Hii ni kati ya
miradi ambayo wananchi wa Lindi na Mtwara wamepata punguzo la bei ya umeme
ambapo kwa sasa wanalipia elfu tisini na tisa tu badala ya laki nne na elfu
hamsini na tano na mwisho wa punguzo hili ni mwezi Desemba mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment