Mwili wa aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow
umeangwa leo jijiniDar Es Salaamtayari kwa kupelekwa mkoani Kilimanjaro
kwa mazishi.
Katika shughuli hiyo Jeshi la polisi limeahidi kuwasaka wahusika
walioshiriki katika tukio la kuuawa kwake na kuwafikisha katika vyombo
vya sheria.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema
wakati wa sala ya kumuaga iliyofanyika katika kanisa katoliki la Ukonga
jijini Dar es Salaam.
Shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu zilihudhuriwa na viongozi
mbalimbali wa serikali pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama ambavyo
vimepata nafasi ya kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu.
IGP Said Mwema alisema juhudi za kuwasaka watu walioshiriki
tukiohilozinaendelea vizuri na hivyo wananchi wanahitaji kutoa
ushirikiano ili kufanikisha suala ambalo linaonekana kurudisha nyuma
kazi ya jeshi la Polisi.
Naye paroko msaidizi wa parokia ya Hananasifu Padre Veri Urio alisema
hakuna mtu mwenye mamlaka ya kutoa uhai wa mwenzake hivyo lazima kila
mtu awe na jukumu la kulinda uhai wake na wa watu wengine.
Marehemu Kamanda Barlow alizaliwa katika kijiji cha Kyou wilaya ya
Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro mwaka 1959 ambapo mwaka 1982 alijiunga
na chuo cha mafunzo cha polisi CCP kwa ajili ya kusomea mafunzo ya
awali ya sheria ya uhamiaji na baadaye kupangiwa katika mkoa wa Mtwara
akiwa kama mkuu wa kituo.
Mwaka 2008 Barlow aliteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara
kabla ya kuteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tabora mwaka 2010
nafasi aliyoshikilia hadi mwaka 2011 alipoteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi
wa mkoa wa Mwanza hadi mauti yalipomfika ambapo ametumikia jeshi kwa
miaka 24.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment