Mwanzoni mwa wiki
tarehe 15 Oktoba 2012 niliwasilisha kwa Katibu wa Bunge kusudio la kuwasilisha
Muswada Binafsi wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Sheria za Hifadhi ya
Jamii (The Social Security Laws (Ammendments) Act wa mwaka 2012 kwa hati ya
dharura kwa mujibu wa Kanuni ya 81 ya Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la Mwaka
2007) iwapo Serikali haitatoa kauli kwa umma ya ratiba ya kupata mapendekezo
toka kwa wadau wa hifadhi ya jamii pamoja na kamati husika ya kudumu ya Bunge
kwa kuzingatia kuwa vikao vya kamati za kudumu za bunge vimeanza tarehe 15
Oktoba 2012 bila suala hilo kuzingatiwa.
Nimefikia uamuzi
huo kwa kuwa mpaka sasa ikiwa zimebaki siku chache Mkutano wa Tisa wa Bunge
kuanza tarehe 30 Oktoba 2012 ambao Serikali iliahidi kuwa italeta marekebisho
ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii, mpaka sasa Serikali haijaitisha mkutano na
wafanyakazi pamoja na wadau wa jamii kupokea mapendekezo hali ambayo inaashiria
upo uwezekano muswada huo usiwasilishwe kwa wakati.
Lengo la Muswada
huo ni kufanya marekebisho yenye kuboresha mfumo wa utoaji wa mafao nchini
ikiwemo kuwezesha kutolewa kwa fao la kujitoa (withdrawal benefits) na mafao
mengine muhimu ambayo hayatolewi katika utaratibu wa sasa wa mifuko mbalimbali
ya hifadhi ya jamii.
Kwa upande mwingine
kufutwa kwa mafao ya kujitoa msingi wake haupo kwenye marekebisho ya sheria
yaliyofanyika tarehe 13 Aprili 2012 pekee bali ni udhaifu katika mfumo mzima wa
kisera na kisheria wa hifadhi ya jamii nchini hali ambayo inahitaji wadau
kutaka mabadiliko makubwa.
Hivyo, Waziri wa
Kazi na Ajira kutoa kauli kwa umma kuhusu maelekezo aliyoyatoa Mamlaka ya
Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) baada ya mkutano wa
nane wa Bunge kufuatia mapendekezo niliyotoa bungeni ya kuitaka Wizara husika
kutoa muongozo wa kisera wa kutengua taarifa kwa umma iliyotolewa ya kueleza
kuwa “kufuatia kuanza kutumika kwa Sheria hiyo (ya 13 Aprili 2012) maombi mapya
ya kujitoa yamesitishwa kwa kipindi cha miezi sita hadi pale miongozo
itakapotolewa ili kuwezesha Mamlaka na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutoa elimu
kwa Wadau”.
Wenu katika
uwakilishi wa wananchi:
0 comments:
Post a Comment