Subscribe:

search

.

Tuesday, 16 October 2012

MKUTANO WA TATHMINI YA UMOJA WA MATAIFA


Balozi wa Kudumu wa Ubalozi wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa, Tuvako Manongi, akizungumza siku ya Jumatatu,wakati wa Uzinduzi wa Tathmini ya Miaka Minne ya Shughuli za Maendeleo za Umoja wa Mataifa ( QCPR). Uzinduzi ambao umefanyika wakati wa Mkutano wa Baraza la Uchumi na Fedha ( ECOSOC)la Baraza Kuu la 67 la Umoja wa Mataifa. Tanzania ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo.

Katika mchango wake Balozi aliwataka wajumbe wa mkutano huo kujadili hali halisi ya matatizo ya kiuchumi , kuongezeka kwa umaskini na upunguaji wa misaada ya kimaendeleo kwa nchi hasa zinazoendelea na nafasi ya Umoja wa Mataifa katika ufadhili na usimamiaji wa miradi ya mendeleo badala ya nchi wanachama kutumia muda mwingi kujitafutia uhalali na umaarufu. Mkutano huo ulifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Jan Eliasson.

0 comments: