|
MEYA WA MANISPAA YA MUSOMA ALEX
KISULULA AKIANGALIA BAADHI YA NYUMBA ZILIZOHARIBIWA NA MVUA KUBWA ZINAZOENDELEA
KUNYESHA MKOANI MARA NA MAENEO MENGINE YA NCHI |
|
WAKAZI WA MTAA WA BUKOBA KATIKA
KATA YA BWERI AMBAO HAWANA MAKAZI KUTOKANA NA NYUMBA ZAO KUEZULIWA NA UPEPO
ULIOAMBATANA NA MVUA KUMBWA |
Mmoja wa wakazi akitoa maelezo kwa Mwandishi wa ITV George Marato
|
JUMLA ya kaya 21, Kata ya Bweri, Manispaa ya Musoma Mkoa wa Mara zimekosa
mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuanguka kutokana na upepo mkali na mvua
kubwa ya mawe iliyonyesha Oktoba 11 mwaka huu.
Waandishi wa habari wakiwa
na Meya wa Manispaa hiyo Alex Kisurura walifika katika eneo lilioharibiwa
ambapo ilishuhudia wakazi wa nyumba hizo wakiwa nje ya nyumba zao huku
wengine wakifanya juhudi ya kukarabati ili kuweza kujisitiri.
Baada ya
kufika eneo hilo baadhi ya wananchi walisema kuwa mvua hiyo kabla ya kunyesha
ulianza upepo mkali pamoja na vumbi kama moshi kasha mvua kubwa iliyoambatana
na mawe.
“Kwanza ulianza upepo mkali ulioambatana na vumbi kubwa kama
moshi kasha ilikuja mvua kubwa iliyonyesha kama saa moja hivi
ambapo ilisababisha nyumba zetu nyingi kuezuliwa na nyingine kuanguka
kama unavyoona,”alisema Matiku Zakaria.
Baada ya mvua hiyo kuisha mali
za wakazi hao hazikujulikana dhamani yake zilikuwa zimeharibiwa vibaya ingawa
hakuna mtu aliyejeruhiwa kwa kuwa mvua hiyo ilinyesha jioni.
Wakazi
walifikwa na maafa hayo ni Matiku Kitogoro, Zakaria Kitogoro, Manyonyi
Kitogoro, Fredrick Ibaso, Albinus Ogono, Kibaso Itinde, Itende Warioba na
Mwalimu Kanoga.
Wengine ni Nyamamba matiku, Joseph Magoti, Ghati Regu,
William Julius, Wambura Itinde, Mashaka Mbeshi, Nyamoko Magoti na Bahati
Itinde na nyumba zingine tano zilizokuwepo katika mtaa wa Rwamlimi katika
kata hiyo.
Diwani wa kata hiyo Shaban Sondobi alisema kuwa baada ya
maafa hayo alipigiwa simu na kwenda kuona uharibifu huo sambamba na
kumtaarifu meya wa manispaa hiyo.
Naye Meya Kisurura amewaagiza
watendaji wa kata hiyo kuwapatia Elimu juu ya ujenzi salama wa nyumba hasa
kipindi hiki ambapo watabiri wa hali ya hewa wametoa taarifa kuwa nchi nzima
itakuwa na mvua kubwa.
“Watendaji ebu anzeni kutoa Elimu kwa wakazi wenu
kabla hawajaanza kujenga na hata hivyo nyumba nyingi tulizotembelea zimechoka
sana lakin pia jitahidini kutoa habari mapema mamlaka husika
panapotokea maafa kama haya.
Kisurura amesema kuwa taarifa tayari
imefika katika kamati ya maafa ya manispaa hiyo ili kufanya tathimini ili
kuweza kuwasaidia wakazi hao lakini pia ametoa rai kwa wananchi wanaoishi
mabondeni kuhama kabla hawajafikiwa na maafa ya mafuriko.
|
0 comments:
Post a Comment