Katika hali isiyokuwa ya
kawaida maiti ya mmoja wa viongozi wa mtandao wa madawa ya kulevya waliokuwa
wakitafutwa sana nchini Mexico Heriberto Lazcano aliyeuawa umeibiwa kutoka
katika nyumba yalikokuwa yakifanyikia mazishi yake.
Rais wa Mexico Felipe
Calderon amelipongeza jeshi kwa operesheni iliyofanikisha kuuawa kwa Lazcano,
aliyekuwa mkuu wa kundi la Zetas ambalo limefanya mauaji ya kikatili, katika
vita dhidi ya madawa ya kulevya nchini Mexico.
Takriban watu elfu 60
wameshauawa katika mgogoro kati ya makundi mbali mbali ya madawa ya kulevya na
polisi tangu Rais Calderon aingie madarakani mwaka 2006.
0 comments:
Post a Comment