KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu, Sheikh Issa Ponda amekamatwa na Jeshi la Polisi usiku wa
kuamkia leo jijini Dar es Salaam. Sheikh Ponda amekamatwa pamoja na
wenzake wapatao 49 wakiwemo wanawake 12, wanaume 37 kwa tuhuma
mbalimbali ikiwemo uchochezi dhidi ya Serikali. Kufuatia tukio hilo,
baadhi ya waislamu mchana huu wameandamana kwenda kituo cha Polisi Kati
kwa ajili ya kushinikiza kuachiwa kwa Sheikh Ponda na waislamu wenzake.
Waandamanaji hao walitawanywa na polisi wakati wakijaribu kuingia
kituoni hapo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment