WANANCHI wa Kata ya Nsalaga katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya,
wamegoma kufanya mkutano wakimshinikiza mkurugenzi wa jiji hilo kumrejesha
aliyekuwa ofisa mtendaji wa kata hiyo, Chripian Matola, aliyehamishiwa Kata ya
Maendeleo ili kujibu tuhuma zinazomkabili
Matola anadaiwa kutumia kinyume cha sheria fedha za ujenzi wa
Shule ya Sekondari ya Uyole zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ukamilishaji
wa ujenzi wa shule hiyo.
Walisema ofisa mtendaji aliyeondoka alikuwa hajasoma mapato na
matumizi kwa takriban miaka miwili iliyopita na kuna fedha za ujenzi wa Shule
ya Sekondari Uyole zilikuwa hazijatolewa taarifa, hivyo isingekuwa rahisi kwa
ofisa mtendaji mpya kujibu maswali ya wananchi.
“Ndugu mwenyekiti, kuna upotevu hapa wa zaidi ya shilingi
milioni tatu ambazo hatujui mtendaji wetu aliyeondoka alizifanyia nini. Tume
iliundwa na kuchunguza sasa leo mnatusomea nini hatutaki …..tunamhitaji yeye
aje asome mwenyewe tumuulize maswali,” alisema Jerry Mwakipesile.
Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni
Diwani wa kata hiyo, Timoth Mandondo (CHADEMA), alilazimika kuahirisha mkutano
na kuwaahidi wananchi kupeleka maombi yao panapohusika.
|
0 comments:
Post a Comment