Friday, 5 October 2012
NINI KINAENDELEA KATI YA SUMAYE NA LOWASA. FUATILIA HAPA.
MGOGORO unaodaiwa kumuhusisha Waziri Mkuu mstaafu, Bw. Frederick Sumaye na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Bw. Edward Lowassa, umechukuwa sura mpya kwa kile kinachoonekana
kila mmoja kumtupia mpira mwenzake.
Juzi gazeti hili lilimpigia simu Bw. Lowassa ili aweze kuzungumzia madai yanayodaiwa kutolewa dhidi yake na Bw. Sumaye, kupitia gazeti moja (si Majira), linalotoka kila siku.
Pia gazeti hili lilimpigia simu Bw. Sumaye kutaka ufafanuzi wa madai yake kwa Bw. Lowassa lakini aliahidi kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam siku chache zijazo.
“Nitawaita waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ili nizungumze kila kitu kuhusu uchaguzi wa NEC, Hanang',” alisema Bw. Sumaye.
Gazeti hilo lilidai, Bw. Sumaye ametangaza vita na Bw. Lowassa kama atawania urais 2015 kwa tiketi ya CCM. Katika majibu yake, Bw. Lowassa alisema yupo kijijini hivyo hafahamu chochote.
Alisema yeye mwenyewe amezisikia taarifa hizo lakini hajalisoma gazeti hilo hivyo hana majibu na kuahidi kutoa ufafanuzi wa madai hayo kesho yake (jana), baada ya kusoma gazeti.
Jana gazeti hili lilimpigia siku Bw. Lowassa ambaye alidai; “Nimesoma magazeti, nimeona walionukuliwa walikuwa ni wasaidizi wake, namsubiri azungumze yeye mwenyewe ili nimjibu.
“Nimesikia leo (jana) kuwa atazungumza na waandishi wa habari, tusubiri azungumze halafu nitamjibu,” alisema Bw. Lowassa.
Alipotakiwa kuzungumzia mgogoro huo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nnauye, alisema unawahusu watu wawili hivyo asingependa chama hicho kihusishwe.
“Waulizeni wao wenyewe msikihusishe chama ambacho hakihusika na mgogoro huo,” alisema Bw. Nnauye.
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Bw. Augustino Mrema alipotakiwa kufafanua mgogoro huo unaweza kuiathiri vipi CCM alidai ni wa kimasilahi na kisiasa.
“Watanzania hawawezi kugawanyika kwa sababu ya mgogoro wa Bw. Lowassa na Bw. Sumaye, tusiwe wajinga wakati wenzetu wanalima, ndugu wakigombana, wewe chukuwa jembe ukalime.
“Kimsingi tunapaswa kuwa macho, tusije kutekwa na mkondo huo, hizo ni siasa za kujipanga, hao ni ndugu wawili hivyo Watanzania wanapaswa kuendelea na shughuli zao za kimaendeleo,” alisema.
Alisema viongozi hao wastaafu wanataka madaraka hivyo wanachokifanya si jambo geni..na majira

Chanzo: Majira
Thursday, 4 October 2012
ZITTO KUMCHANGIA MJANE WA MWANGOSI NA WANAE BIMA YA AFYA
KATIKA siku ya mwisho ya harambee ya kumchangia mjane wa marehemu Daud Mwangosi, Ndugu Zitto Kabwe amejitolea kumchangia mjane wa marehemu kwa kumlipia ada ya uanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Kijamii (NSSF) kwa kila mwezi na kwa miaka mitatu mfululizo.
" Nimeona nami niunge mkono harambee hii. Pamoja na michango ya fedha iliyotolewa kumsaidia mjane kuanzisha mradi wa kujikimu, mimi naona ni muhimu pia mjane akawa na hakika ya huduma ya afya yake na watoto wake wanne. Hivyo, mchango wangu utakuwa ni kwenye eneo hilo la Bima ya Afya na kwa miaka mitatu." Anasema Zitto Kabwe alipoongea na Mjengwablog.com, mtandao wa Kijamii ulioratibu harambee ya mjane wa Daud Mwangosi.
Hii ni mara ya pili kwa Ndugu Zitto Kabwe kuchangia kwenye masuala ya kijamii kupitia mtandao wa kijamii wa Mjengwablog.com, mara ya kwanza ni alitoa mchango wake pale Mtandao wa Mjengwablog.com ulipoendesha harambee ya kuwachangia watoto wa Somalia waliokuwa katika hatari ya kufa kwa njaa. Katika harambee iliyomalizika Jumapili ya Septemba 30 mwaka huu na iliyochukua kipindi cha mwezi mmoja,zaidi ya shilingi milioni tano na nusu zimekusanywa.
Mchango huo wa Ndugu Zitto Kabwe una maana mjane wa marehemu ataweza kuwa na hakika ya yeye na watoto wake wanne kupata huduma za afya bila kufikiria malipo kwa kipindi cha miaka mitatu. Baada ya hapo,michango ya mjane huyo ya kila mwezi kwa mfuko huo wa hifadhi ya kijamii ( NSSF) ambayo atakuwa akilipiwa na Ndugu Zitto Kabwe itakuwa ni malimbikizo ya akiba yake ambayo mjane atakuwa na uwezo wa kuichukua kama akipenda. Kwa sasa mjane wa Daud Mwangosi hayuko kwenye utaratibu wowote wa Bima ya Afya, kwake yeye na wanawe.
Harambee ya mjane wa Daud Mwangosi iliyoendeshwa kwa uwazi kwa njia ya MPESA, TigoPesa, Airtel Money, NMB Mobile na Western Union ilimwezesha mchangiaji kuliona jina lake na mchango wake kwenye orodha ya wachangiaji iliyokuwa ikiwekwa mtandaoni kila siku.
Michango ilikuwa ni hiyari, hakuna aliyeombwa kutoa na utaratibu haukuruhusu ahadi za kuchangia, bali, mwenye nacho alitoa na hapo hapo kuorodheshwa kama mchangiaji. Utaratibu haukuruhusu pia michango iliyofungamana na siasa za vyama.
Hatua hiyo ya uwazi na kutanguliza ubinadamu na si itikadi kwenye uchangiaji imechangia kupelekea Watanzania wengi wa kada zote, kwa namna moja au nyingine kushiriki kwenye kuchangia. Kuna waliochangia shilingi elfu moja na kuna waliochangia mpaka shilingi milioni moja.
Ari hii ya Watanzania kujitolea kusaidiana kwenye hali kama iliyomkuta mjane wa Daud Mwangosi imedhihirisha umoja na upendo tulionao kama Watanzania, na pia imeonyesha jinsi tunavyoijali amani yetu na hivyo jamii, kupitia michango hii, imeonyesha pia kwa vitendo, dhamira ya kulaani kwao vitendo vya maovu na vinavyotokana na matumizi ya nguvu yasiyo ya lazima kama kile kilichomtokea mwandishi Daud Mwangosi.
Baadhi ya watu maarufu katika jamii waliojitokeza kwa hiyari yao kumchangia mjane wa Daud Mwangosi kupitia mtandao wa kijamii wa Mjengwablog.com ni pamoja na Shy- Rose Bhanji, Ananilea Nkya, John Bukuku ( Mmiliki wa Fullshangwe.blog) na Ndugu Mobhare Matinyi aliyepata kuwa mhariri wa gazeti la Majira.
Michango kwa mjane wa Daud Mwangosi itaingizwa kwenye akaunti ya mjane ya CRDB, Iringa leo alhamisi, Oktoba 4, 2012. Vielelezo vya kibenki vitawekwa kwenye mtandao wa Mjengwablog.com kwa kila mmoja kuona jumla iliyowasilishwa kwa mjane na orodha ya majina ya wachangiaji.
Chanzo: Maggid Mjengwa, Mjengwablogspot.com
SABABU ZILIZOMUANGUSHA WAZIRI MKUU MSTAAFU FREDERICK SUMAYE ZATAJWA
SIASA za makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), zimetajwa kuwa chanzo cha kuangushwa kwa Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye katika nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), kupitia Wilaya ya Hanang’ Mkoa wa Manyara.
Sumaye ambaye anatajwa kuwa ana nia ya kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu ujao, alishindwa na Dk Mary Nagu ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji).
Katika uchaguzi huo, Sumaye alipata kura 481 dhidi ya Nagu, aliyepata kura 648. Mbali na Sumaye, wajumbe wengine waliokuwa wakimuunga mkono akiwamo Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, Goma Gwantu, pia walishindwa katika uchaguzi huo.
Dalili za kushindwa kwa Sumaye, ambaye alikuwa akiungwa mkono na wajumbe wa kamati ya siasa ya CCM wa wilaya hiyo, zilianza kuonekana wiki moja kabla ya uchaguzi huo. Kambi ya Dk Nagu ambayo inatajwa kwamba inaungwa mkono na kambi ya Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, ilionekana kuwa na “ushawishi” mkubwa katika vikao vya kamati ya siasa ya mkoa na kwenye Kamati Kuu ya CCM. Hali hiyo, ilitokana na ukweli kuwa Dk Nagu kama taratibu ambazo zilihitajika, hakupewa baraka na kamati ya siasa ya wilaya hiyo, kugombea kwa kile ambacho kilielezwa kukwepa mpasuko wa CCM Hanang' na pia kumpa heshima Sumaye.
Hata hivyo, habari zimeeleza kuwa tofauti na msimamo wa Kamati ya Siasa ya wilaya hiyo, Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Manyara, ilionekana kumuunga mkono Dk Nagu hasa kutokana na ukweli kuwa karibu nusu ya wajumbe wa kamati hiyo walikuwa wagombea.
Kikao cha kamati ya siasa ya mkoa, licha ya kurejesha jina la Dk Nagu pia, kilipendekeza kuondolewa majina ya wagombea kadhaa katika wilaya ya Hanang' likiwamo jina la Mwenyekiti wa wilaya hiyo, Goma Gwaltu ambaye alikuwa kambi ya Sumaye.
Taarifa za kupendekezwa kuondolewa majina ya wanaomuunga mkono Sumaye, zilitolewa na baadhi ya wajumbe wa Wilaya ya Hanang’, lakini hata hivyo, Katibu wa CCM Mkoa wa Manyara, Ndeng'aso Ndekubali alizikanusha. “Kamati ya siasa ya mkoa ni kikao cha siri na nadhani ni mapema mno kulalamikia suala hilo, ni vyema wakasubiri uamuzi wa juu, ” alisema Ndekubali. Hata baada ya kurejeshwa majina na Nec, ilibainika kuwa wagombea ambao Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo, iliwapa alama za chini, wamerejeshwa katika mchakato wa uchaguzi.
Dalili za kuanguka Sumaye, pia zilijionyesha siku ya kupiga kura, ukumbini na nje ya ukumbi kutokana na wajumbe waliokuwa wanamuunga mkono Dk Nagu kuwa na uhakika mkubwa wa ushindi. Wakati wa kujieleza ili aombe kura, Sumaye ambaye alionekana kama tayari amebaini nguvu ya Dk Nagu, alieleza kushangazwa na uamuzi wa Dk Nagu kugombea nafasi hiyo, hali ya kuwa ni waziri.
Sumaye, pia alikemea kile alichodai kuwa ni rushwa kwenye chaguzi za CCM na kuahidi kama akichaguliwa, angeshirikiana na viongozi wenzake kuhakikisha anawachukulia hatua kali watoa rushwa. Awali Dk Nagu katika maelezo yake, alitumia fursa ya kuomba kura kukanusha kuwa anatumiwa na kundi la Lowassa ili kumkwamisha Sumaye.
Dk Nagu alifafanua kuwa yeye kama Mbunge wa Hanang’ na Waziri, kamwe hawezi kutumiwa na kundi fulani kwa masilahi ya makundi kwani hata yeye ana sifa za kuchaguliwa. Wakati wa maswali, Dk Nagu hakuulizwa wakati Sumaye aliulizwa maswali matatu ambayo aliyajibu kwa ufasaha, lakini hakuchaguliwa.
Mwenyekiti wa CCM aliyeshindwa, Goma Gwaltu, alieleza kupinga mambo kadhaa yaliyokiukwa katika uchaguzi, lakini hata hivyo, alisisitiza kujiandaa kutoa tamko rasmi. “Nitazungumza siku si nyingi kuelezea uchaguzi huu,” alisema Gwaltu.
Naye Sumaye kwa upande wake, alisema anakusudia kuzungumzia yaliyojiri katika uchaguzi huo hivi karibuni. “Naomba uwe na subira, nitawaita wanahabari na tutazungumza. Leo (jana) nimepigiwa simu na waandishi kama 50, wote nimewaambia kuwa nitazungumza siku chache zijazo,” alisema Sumaye.
Mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Rose Kamili ambaye kwa muda mrefu alikuwa diwani kwa tiketi ya CCM kabla ya kuhamia Chadema, alieleza kuwa Sumaye aliangushwa kwa nguvu ya fedha. Alisema kuwa kitendo cha Sumaye kutajwa kuwa anataka kuwania urais katika uchaguzi ujao ndiyo sababu ya kutoswa katika uchaguzi huo ili kupunguza ushindani. Kwa upande wake Gwaltu alisema kilichomwangusha Sumaye ni makundi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Alisema kuwa makundi hayo ambayo yameanza kujipanga kwa ajili ya kushinda katika kinyang’anyiro cha kuwania urais, yalifanya kila njia kuhakikisha kuwa Sumaye hapenyi katika hatua hiyo, lengo likiwa ni kufanya upinzani kuwa mdogo 2015.
Kada mkongwe wa chama hicho ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Basotu, Samwel Kawoga alisema kuwa makundi hayo yalianza kuonekana wazi siku chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo. Alisema kuwa makundi hayo ni pamoja na yale yanayoongozwa na makada wa chama hicho wanaoutaka urais na mengine ni yale yanayoibuka kila unapofanyika uchaguzi ndani ya chama hicho.
Mujjahidina wavamia makaburi Mkoani Pwani wakitaka Kaburi la Aruina Rolan Lifukuliwe
NA MWANDISHI WETU, BAGAMOYO
KUNDI la waumini wa dini ya Kiislamu (Mujjahidina), kutoka Msikiti wa Majani Mapana Tandika, wilayani Bagamoyo, mkoa wa Pwani, limefanya vurugu kubwa baada ya kuvamia makaburi ya Kiislamu na kutaka kaburi alilozikwa mtoto Aruina Rolan Mitaban lifukuliwe.
Waislamu hao, ambao walionekana kujawa na jazba, walidai mwili wa mtoto huyo, hauruhusiwi kuzikwa katika maeneo yao, kwa sababu ni Mkristo.
Tukio hilo lilitokea Septemba 30, mwaka huu, ikiwa ni mwezi mmoja baada ya kuzikwa kwa mwili wa mtoto huyo, katika makaburi hayo.
Tukio hilo, limeonekana kuibua hisia kali kwa wakazi wa Bagamoyo, ambao miongoni mwao walidai huo ni unyama wa kupindukia.
“Haiwezekani kaburi la mtoto kama yule, malaika wa Mungu asiyejua kitu, linakwenda kufukuliwa kinyama vile… nadhani tunakoelekea ni kubaya sasa,” alisema Suleiman Wahid.
“Huwezi kusambaratisha kaburi namna hii, ilitakiwa wakutane na viongozi wa makaburi kwanza, marehemu yule ana kosa gani? Watanzania tunapotea,” alisema Wahid.
Kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, aliamua kuitisha kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha dharura ili kujadili.
Baada ya kuitisha kikao hicho, aliziita pande mbili zinazohusika, ili kupata ufumbuzi wa suala hilo.
Kipozi aliwataka waumini wa dini hizo na wakazi wa wilaya hiyo, kujenga tabia ya kuvumiliana pale kunapokuwa na matatizo, badala ya kuendekeza jazba na hasira ambazo haziwezi kuleta tija.
Mara baada ya kikao hicho cha kamati ya ulinzi na usalama, upande wa marehemu huyo wakiongozwa na baba wa marehemu, Rolan Mitaban, Oktoba 2, mwaka huu walilazimika kwenda kufukua mwili huo wa marehemu na kwenda kuuzika upya jijini Dar es Salaam.
“Tukio hili limetokea, nikalazimika kuitisha kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama, na pande zote zinazohusika.
“Moja ya maazimio tuliyokubalina ni kwamba, kaburi lile lisibughudhiwe na mtu yeyote na ndugu zao walijengee kama yalivyojengewa makaburi mengine.
“Lakini katika hali ya kushangaza, nimesikia jana baba mzazi wa marehemu akiwa na ndugu zake, waliamua kwenda kufukua mwili wa marehemu na kwenda kuuzika Dar es Salaam,” alisema Kipozi.
Kutokana na tukio hilo, DC Kipozi alitoa wito kwa viongozi wa dini, kuhakikisha wanawasiliana na ofisi yake, ili kushughulikia matatizo ya aina hiyo yanapojitokeza, ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kutokea.
Baadhi ya ndugu wa marehemu, ambao waliomba majina yao yahifadhiwe, walisema kitendo kilichofanywa na waumini wa dini ya Kiislamu si cha kiungwana, kwani kama kulikuwa na tatizo hilo, walipaswa kuwataarifu wahusika ili waweze kwenda kushughulikia kwa kufuata sheria.
Hii ni mara ya pili kutokea kwa vurugu katika makaburi ya Tandika, itakumbukwa mwanzoni mwa mwaka huu, kuliibuka uvumi kuwa kuna joka kubwa la kishirikina katika makaburi hayo na kupelekea mganga wa kienyeji maarufu Zoazoa, kwenda kuweka matambiko ambayo hayakuzaa matunda.

Chanzo: Mtanzania
Wednesday, 3 October 2012
HIVI NDIVYO HALI ILIVYOKUWA KATI YA YANGA NA SIMBA. MCHEZO ULIISHA KWA KUTOSHANA NGUVU SIMBA 1 YANGA 1
Mashabiki wa timu ya Yanga walikuwa na hamu ya angalau kurudisha magoli 5 waliyofuwngwa na watani wao Simba hata hivyo wamefanikiwa kutoka sare na kutoshana nguvu katika mchezo huo
NCHI INA UPUNGUFU WA TANI 150,000 ZA SUKARI. HIVI HII INAPASWA KUTOKEA KATIKA NCHI KAMA TANZANIA KWELI?
Aswin Rana, Chairman Speaking
Participant atended Conference TSPA,
Deputy Minister for, Agriculture and Food Security,(FSSP) Adama Malima addreses whe the opening the Conference, Federation Of SADC Sugar Producers held Dar es Salaam Kunduch Beach Hotel
Mwandishi Wetu
SERIKALI imesema nchi inakabiliwa na uhaba wa sukari tani 150,000 kila mwaka kutokana na uwezo wa viwanda hapa nchini kuzalisha tani 350,00 wakati mahitaji ni tani 500,000 kwa mwaka.
Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima alipokuwa akifungua mkutano wa wazalishaji wa sukari kutoka nchi za Jumuiya ya Uchumi Kusini mwa Africa(SADC), unaoendelea jijini Dar es Salaam Malima alisema kiasi hicho ambacho ni pungufu imekuwa ngumu kukipata kutoka nchi nyingine kwa kuwa nazo zinahitaji sukari kwa wingi.
“Sisi hatuzalishi sukari kwa kiwango cha kutosha, tuna mahitaji ya sukari tani laki tano kwa mwaka sisi tunazalisha tani laki tatu na hamsini hivyo tuna uhaba wa tani laki moja na nusu ambayo nayo ni ngumu kuipata kutoka kwa wenzetu,”alisema Malima.
Alisema kutokana na hali hiyo Serikali inaweka mkakati ya kutaka uzalishwaji wa sukari ufikie tani milioni moja kwa mwaka ndani ya miaka sita ijayo.
“Kutokana na hilo wadau wa sekta hii ni muhimu wakajipanga ili kuhakikisha lengo hilo linatimia,”alisema na kuongeza;
“Tunaangalia maeneo muhimu ya uzalishaji wa miwa ambayo ndiyo inatumika kutengeneza sukari ili kufanikisha hilo.”
Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Wazalishaji wa Sukari Tanzania(TSPA), Balozi Fadhili Mbaga alisema kwa mwaka huu wanategemea kuzalisha sukari kiasi cha tani 320,000 kwa kuwa msimu ni mzuri.
“Mwaka jana tulizalisha tani 80,000 ambayo ilikuwa ni kidogo ila mwaka huu tunatarajia kuzalisha kiasi kikubwa ambacho bado kitakuwa hakitoshi kwa matumizi ya hapa nchini,”alisema Balozi Mbaga.
Alisema hivi sasa nchi za SADC zinazalisha wastani wa tani milioni tano za sukari kwa mwaka ambayo ni asilimia 3 ya uzalishwaji wa sukari duniani.
Mkutano huo umehudhuriwa na nchi ya Angola, Botswana, Lesotho, Malawi, Mauritius, Musumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Swaziland, Tanzania, Zambia na Zimbabwe.
KARIBU UWASAIDIE WATOTO WENYE MATATIZO YA MOYO
Taasisi ya Lions Club ya jijini Dar es Salaam inaendesha zoezi la kukusanya michango ya fedha kwa ajili ya kuwasaidia watoto wasio na uwezo wenye matatizo ya moyo kupata matibabu. Unaweza kutoa mchango wako hata kwa njia ya hundi kuiongezea nguvu Lions Club. Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na Rais wa Lions Club Nimira Gangji kwa nambari +255715979966.
RAIS JK AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO NA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA BAN KI MOON.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani, wakati wa uzinduzi wa mpango wa pili wa Ubunifu wa Uboreshaji wa Huduma za Afya ya Mama na Mtoto, katika maeneo ya vijijijni Nchini Tanzania, mpango huo wa miaka mitatu unafadhiliwa na wafadhili wawili, Meya ya Jiji la New York na philanthropies Michael Bloomberg na Dr. Helle Agerup ambapo wamechangia dola za kimarekani milioni 15 kutoka kushoto ni Meya wa jiji la New York Michael Bloomberg, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, na Dr, Helle Agerup
Meya Michael Bloomberg, Ban Ki Moon, Rais Jakaya Kikwete na Dr. Hellen wakiangalia video fupi iliyokuwa ikionyesha kazi zilizofanywa za ukoaji wa akina mama wajawazito kwa kuwapatia huduma ya upasuaji wa dharura, huduma ambayo imepatika kwa ufadhili wa Meya na Philanthropies Michael Bloomberg ambapo kwa kupitia ufadhili alioufanya kuanzia mwaka 2006 zaidi ya wataalam 106 wakiwamo wakunga na manesi wamepatiwa mafunzo ya upasuaji wa dharura, pia huduma za afya zimeboreshwa kwa kujenga au kuvifanyia ukarabati vituo vya afya na zahanati katika ngazi za vijiji katika maeneo ya mikoa ya Pwani, Morogoro na Kigoma. Ufadhili na kazi kubwa iliyofanywa na Bloomberg pamoja na juhudi za Rais Jakaya Kikwete zimemvutia Dr. Hellen naye kuwekeza nchini Tanzania.
Rais Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni anayetizama pembeni ni Katibu Mkuu Ban Ki Moon
Rais Jakaya Kikwete akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo yake na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ambaye naye aliongoza ujumbe wake. Matukio hayo yote yamefanyika siku ya Jumanne katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Jijini New York, Marekani.
Chanzo:Mjengwa.blogspot.com
BAADA YA BEI YA PETROLI KUSHUKA GHAFLA HIVI NDIVYO HALI ILIVYO KATIKA VITUO VYA MAFUTA VINGI
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetoa bei kikomo mpya ambazo zitaanza kutumika leo nchini kote ikiwa imeshuka kwa Sh 306, kwa lita ya petroli, Sh 192 kwa lita moja ya dizeli huku mafuta ya taa bei ikibaki bila kubadilika.
Taarifa iliyotolewa jana na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo, ilisema bei za mafuta ya petroli kwa Dar es Salaam itakuwa Sh 1,994 kwa lita moja ikiwa imeshuka kutoka Sh2,300 ya bei ya Septemba. Alisema mafuta ya dizeli bei yake imeshuka hadi kufikia Sh1,950 kutoka Sh2,142, wakati mafuta ya taa yanabakia Sh1,993 kutokana na kutoingia meli yoyote ya mafuta hayo.
Taarifa hiyo ilisema bei hizo, zitaendelea kuongezeka kutokana na gharama za usafirishaji kutoka Dar es Salaam kwenda mikoani, ingawa kwa ujumla katika kila eneo punguzo litakuwa ni Sh 306 na Sh 192 kwa petroli na dizeli kwa kila lita moja. “Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko na Ewura itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta,”alisema na kuongeza; “Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya uamuzi stahiki kuhusu ununuzi wa bidhaa za mafuta kulingana na bei anayoiona mteja inamfaa.”
Kaguo alisema kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziwe chini ya bei kikomo na kama mfanyabiashara atakiuka atapewa adhabu ya kulipa Sh3 milioni. Pia alivitaka vituo vyote vya mafuta kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana ili mteja afanye uchaguzi wa kununua mafuta akiwa anajua bei halisi ya mafuta katika kituo husika. “Wanunuzi wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi ya malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita kwani stakabadhi hiyo ya malipo itatumika kama kidhibiti cha ununuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo; ama endapo utakuwa umeuziwa mafuta yenye kiwango cha ubora kisichofaa,” aliongeza Kaguo.
Hivi karibuni Baraza la Ushindani wa Haki (FCC), lilitupilia mbali rufani ya kampuni 13 zinazojishughulisha na uuzaji wa mafuta, zilizokuwa zinapinga kanuni mpya ya kukokotoa bei za mafuta iliyobuniwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura). Katika hukumu hiyo iliyotolewa wiki iliyopita, Mwenyekiti wa baraza hilo, Razia Sheikh, alisema uamuzi wa kuitupa rufani hiyo ulitokana na warufani, kushindwa kuthibitisha madai yao kikamilifu.
Alisema baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili, baraza liliridhika kuwa Ewura ilikuwa imefuata taratibu zote zilizowekwa kisheria, kabla ya kutangaza kanuni mpya za kukokotoa bei za mafuta nchini. Katika usikilizaji wa shauri hilo, Mwenyekiti Sheikh alisaidiwa na wajumbe wawili ambao ni Malima Bundala na Ali Juma.
Kampuni zilizokata rufaa ya kupinga uamuzi wa Ewura ni pamoja na BP Tanzania Limited, Engen Petroleum Tanzania Limited, Camel Oil Tanzania Limited, Oilcom Tanzania Limited, Total Tanzania Limited, Gapco Tanzania Limited na Hass Petroleum Tanzania Limited. Nyingine ni Orxy Oil Company Limited, MSG International Tanzania Limites, GBP Tanzania Limited, Lake Oil Limited, Moil Tanzania Limited and Acer Petroleum Tanzania Limited. Pamoja na kutupilia mbali rufani hiyo, Sheikh pia aliziamuru kampuni hizo kulipa gharama za kesi.
Kwa mujibu nyaraka za baraza hilo, gharama za mawakili wa Ewura peke yake ni zaidi ya Sh100 milioni. Pamoja na mambo mengine, kampuni hizo zililiomba baraza hilo kuifuta kanuni hiyo mpya kwa vigezo kuwa, Ewura haikufikiria mambo kadhaa kabla ya kuitangaza.
Chanzo:Mwanachi.co.tz
BREAKING NEWS: BWENI LA CHUO CHA KILIMO NALIENDELE-MTWARA LATEKETEA KWA MOTO
Habari za kusikitisha zimelifikia dawati letu la habari hivi punde kuhusu kuungua kwa baadhi ya Majengo ya Chuo cha Kilimo cha Naliendele Mtwara. Mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho amesema kuwa hadi sasa moto bado unaendelea ila Wafanyakazi wa zima moto wa Bandari na Airport wamefika eneo la tukio ingawa wamechelewa kufika kwa saa moja zaidi, Mwanafunzi huyo amesema hadi sasa ni bweni la Wasichana tu ndio lililoathirika. Chanzo cha moto huo hakijafahamika hadi sasa, na tumeshindwa kujua kama kuna majeruhi au ni hasara ya kiasi gani imetokea.
Endelea kufuatilia blog hii kwa taarifa zaidi.
Chanzo: Afrokija
Subscribe to:
Posts (Atom)