Mkuu
wa mkoa wa Arusha Mh.Magesa Mulongo akisalimiana na baadhi ya viongozi
wa Jeshi la Polisi wa Mkoa huu mara baada ya kuwasili katika kiwanja cha
michezo kilichopo katika moja ya kambi zilizopo mkoani humo, kulia
kwake ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha (ACP) Liberatus Sabas
akimtambulisha viongozi hao.
Mkuu
wa mkoa wa Arusha Mh. Magesa Mulongo akikagua gwaride lililoandaliwa na
jeshi la Polisi mkoani humowakati wa hafla ya makabidhiano ya vyeti kwa
askari 37 wa mkoa huu waliofanya vizuri zaidi katika utendaji wao wa
kazi za kila siku. Hafla hiyo ilifanyika tarehe 08/10/2012 katika
kiwanja cha michezo kilichopo katika moja ya kambi ya jeshi hilo iliyopo
Mjini Arusha.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Arusha (ACP) Liberatus Sabas akimkaribisha mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Magesa Mulongo ili aweze kutoa vyeti na
fedha taslimu Tsh laki moja kwa kila askari ambaye alikuwa amefanya
vizuri zaidi katika utendaji wake wa kazi za kila siku.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mh. Magesa Stanslaus Mulongo akimkabidhi cheti cha
utendaji bora wa kazi askari wa jeshi la Polisi mkoani humo Mkaguzi
Msaidizi wa Polisi Jane Warioba wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika
kiwanja cha michezo kilichopo katika kambi ya polisi ya Mjini Arusha
tarehe 08/10/2012.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mh.Magesa Mulongo akitoa pongezi kwa askari wote wa
Jeshi la Polisi mkoani humo kutokana na utendaji mzuri wa kazi zao za
kila siku katika hafla ya kuwatunuku askari 37 wa jeshi hilo mkoani hapa
ambao walifanya vizuri zaidi iliyofanyika katika kiwanja cha michezo
kilichopo katika moja ya kambi zilizopo mjini hapa tarehe 08/10/2012.
Baadhi
ya askari wa Jeshi la Polisi mkoani A warushakiwa katika picha ya
pamoja mara baada ya kunukiwa vyeti na fedha taslimu Tsh laki moja kila
mmoja kutokana na utendaji mzuri wa kazi zao za kila siku.
0 comments:
Post a Comment