Itakumbukwa
kuwa wakati wa Mkutano wa Nane wa Bunge uliofanyika kuanzia Juni –
Agosti, 2012, Spika wa Bunge aliunda Kamati Ndogo ya Haki, Kinga na
Madaraka ya Bunge kuchunguza tuhuma zilizokuwepo kuwa Wajumbe wa Kamati
ya Bunge ya Nishati na Madini na baadhi ya Wabunge walijihusisha na
Vitendo vya rushwa wakati wa mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya
Nishati na Madini (2012/2013).
Hivyo,
Tangazo hili linatolewa kuuarifu Umma kwamba Kamati hiyo Ndogo
imekamilisha kazi yake kama ilivyoelekezwa kwenye Hadidu za Rejea na
kukabidhi Taarifa ya Uchunguzi huo kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano tarehe 27 Septemba, 2012.
Kwa
mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Spika atatoa muongozo
kuhusu utaratibu wa kufuata kuhusu uwasilishaji wa Taarifa hii Bungeni
ambapo yaweza kuwa Spika akatoa uamuzi ama Kamati kuwasilisha Taaarifa
hiyo Bungeni.
Spika
atatoa taarifa ya kukamilika kwa uchunguzi huo Bungeni wakati wa
Mkutano wa Tisa wa Bunge unaotarajia kuanza tarehe 30 Oktoba, 2012.
Imetolewa na:
Ofisi ya Bunge
S.L.P. 9133
DAR ES SALAAM
0 comments:
Post a Comment