Waislamu
nchini Uganda mwaka huu hawatoweza kuhudhuria ibada ya kwenda kuhiji
Makka baada ya utaratibu wa kuwapatia Visa kucheleweshwa kwa kuhofia
ugonjwa hatari wa Ebola.
Akizungumzia
suala hilo Balozi wa Saudi Arabia amesema kuwa kufikia Oktoba 4 wakati
Shirika la Afya Duniani linatangaza Uganda kuwa huru dhidi ya ugonjwa
huo, ilikuwa umebakia muda wa siku 5 tu kukamisha zoezi la kushughulikia
mahujaji wa kigeni, muda ambao usingetosha kutoa viza kwa mahujaji wa
Uganda.
Balozi
Jamal Abdul Aziz Raffa amesema japokuwa mahujaji wa Uganda
hawakufanikiwa kwenda kuhiji, lakini bado wanastahili kuitwa Hajjs na
Hajjats kwa sababu walikwisha jiandaa kufanya hijja hiyo.
Ameongeza
kuwa Ubalozi huo umesitisha pia kutoa viza kwa wafanyabiashara wa
Uganda wanaotaka kuelekea Saudi Arabia mpaka hapo watakapojiridhisha
kuwa sasa hali ni shwari.
Jumla ya mahujaji 900 walikuwa wamejiandikisha kwa safari ya Makka mwaka huu.
Hii
ni mara ya pili katika kipindi cha miaka 12 mahujaji wa Uganda
wanashindwa kwenda Saudi Arabia kuhiji kutokana na tatizo la Ebola.
Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2001 wakati ugonjwa huo hatari ulipoikumba wilaya ya Gulu.
0 comments:
Post a Comment