Bunge la Afrika liliundwa mwaka 2004
sambamba na kuasisiwa Umoja wa Afrika AU na linahesabiwa kuwa ni
miongoni mwa nguzo muhimu za umoja huo. Lengo la kuundwa bunge hilo ni
kutoa fursa kwa wawakilishi wa nchi zote wanachama kukutana na
kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali na kutoa ushauri
kwa nchi za Afrika.
Bunge la Afrika lina wajumbe 265 ambao
huchaguliwa na mabunge ya nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. Hata hivyo
Bunge hilo la Afrika halina nguvu za kutunga sheria bali kazi yake ni
kutoa ushauri tu.
Rais Boni Yayi wa Benin ambaye nchi yake
ndiye mwenyekiti wa hivi sasa wa Umoja wa Afrika ameahidi kuunga mkono
juhudi za kuliimarisha zaidi Bunge la Afrika.
Alisema jana usiku wakati wa kuanza kazi
rasmi bunge hilo huko Johannesburg, Afrika Kusini, kwamba, nchi zote za
Afrika zinapaswa kuunga mkono jitihada za kulifikisha bunge hilo katika
kiwango cha juu cha hadhi ya bara la Afrika.
0 comments:
Post a Comment