Aliyekuwa
mgombea nafasi ya Uenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Mara, Gabriel
Mnasa Sabi ameuomba uongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja
na Umoja wa Vijana makao makuu, kuingilia kati chaguzi za umoja ambazo
zimetawaliwa na vitendo vya hujuma na rushwa.
Sabi
ambaye juzi aishindwa kwa tofauti ya kura 14 dhidi ya Ditu Manko ,
alisema kuwa uchaguzi wao haukuwa huru na haki kwani matokeo
yalijulikana kabla ya kupiga kura.
Alisema
kuwa alitangaziwa matokeo hayo wakati wa kampeni kwa madai kuwa nafasi
ya uenyekiti lazima itoke wilaya ya Tarime kutokana na nguvu ya kifedha.
“Hali
hiyo ilinifanya kunyong’onyea hata kabla ya uchaguzi, hata hivyo
nilipiga moyo konde na kuingia kwenye uchaguzi, matokeo yakawa yaleyale,
nilishangazwa sana na wafuasi wangu wakaamua kutoendelea na uchaguzi
huo,” alisema Sabi.
Alisema
kuwa baada ya matokeo hayo, fujo zikaanza kwani wafuasi wake walichoka
kuona vitendo vya uonevu vya waziwazi na kuongeza kuwa pamoja na wafuasi
wake kutoka, uchaguzi huo uliendelea na kuhoji hao waliochaguliwa
walipata kura hizo kwani sidhani kama idadi ya wapiga kura kwa mujibu wa
katiba ilifikiwa.
“Kasoro
hizi si za kuziacha kwani zinawagawa wanachama, ni lazima zikemewe
kwani bado kuna chaguzi nyingi ndani ya chama,” alisema.
Alifafanua
kwa kusema kuwa hana tatizo na uongozi wa juu wa CCM kutokana na sera
madhubuti zenye kuleta maendeleo ya nchi, ila kilio chake ni viongozi
wanaokipaka matope chama hasa wa ngazi ya chini.
0 comments:
Post a Comment