Mbunge wa viti maalum (CCM)
mkoa wa Singida Diana Mkumbo Chilolo akiwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa
UWT mkoa wa Singida kwa kumchagua tena kuwa mwenyekiti wao kwa kipindi cha
miaka mitano ijayo.Chilolo alipata kura 431 dhidi ya kura 451 zlizopigwa.
Diana Mkumbo Chilolo ametetea kwa kishindo nafasi yake kama Mwenyekiti
wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT (CCM) mkoa wa Singida baada ya kupata kura
431 dhidi ya 451 zilizopigwa.
Kwa ushindi huo, Chilolo ambaye pia ni mbunge wa viti maalum mkoani
Singida amewaacha kwa mbali wapinzani wake Pendo Kone aliyepata kura 11 na
mwalimu Sundi Samike aliyeambulia kura nane.Msimamizi wa mkutano huo mkuu wa uchaguzi Dkt. Parseko Kone amemtangaza
mkuu wa wilaya ya Manyoni Fatuma Towfiq kuwa amaechaguliwa katika nafasi ya
mjumbe wa baraza kuu taifa UWT. Amesema mfanyakazi wa TANROADS mkaoni Singida Sara Mkumbo,
amememgaragara vibaya mpinzani wake Mwajuma Shaa kwa kura 247 dhidi ya kura
153.
Dkt. Kone ambaye ni mkuu wa mkoa wa Singida amewataja washindi wa
baraza la UWT kutoka wilaya ya Singida vijijini kuwa ni Halima Kundya na Debora
Andrew.
Amesema kutoka wilaya ya Ikungi ni Mariamu Limu na Tatu Dahani, wilaya
ya Iramb ni Monica Samwel na Elimaba Lula, wilaya ya Mkalama ni Mariamu Kahola
na Helena Kitila, Manispaa Singida ni Aisha Matembe na Sara Mkumbo wakati
wilaya ya Manyoni ni Magreth Mlewa na Rehema Chizumwa.
Aidha Dkt. Kone amesema Hadija Nyuha ameshinda nafasi ya uwakilishi wa
jumuiya ya wazazi kwenye mkutano mkuu wa UWT, wakati Mwakilishi wa UVCCM ni
Janet Mughwai.
Jane Kishari amechaguliwa kuwa mjumbe kwenye mkutano mkuu wa CCM mkoa.
0 comments:
Post a Comment