Subscribe:

search

.

Monday, 8 October 2012

WFP NA VODACOM ZATUMIA TEKNOLOJIA



 Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa mradi wa majaribio wa uwezeshaji wanawake wajawazito na watoto mkoani Mtwara kupata fedha za kununua chakula chenye lishe. Walengwa watakuwa wakipokea fedha kila mwezi kupitia mtandao wa M-PESA. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.

Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan (katikakati)akisisitiza jambo kwa  waandishi wa habari wakati wa utambulisho wa mradi wa majaribio wa uwezeshaji wanawake wajawazito na watoto mkoani Mtwara kupata fedha za kununua chakula chenye lishe. Walengwa watapokea fedha hizo kupitia huduma ya M-pesa. Wengine pichani ni Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule na Ofisa lishe wa WFP Rosemary Mwaisaka.

Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan,wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu ushirikiano wa Vodacom Tanzania na WFP katika mradi wa uwezeshaji wanawake wajawazito  fedha za kununulia chakula chenye lihse mkoni Mtwara.  Fedha hizo hutumwa kupitia huduma ya M-pesa.
 

0 comments: