Friday, 24 August 2012
SENSA YA LIWALO NA LIWE
Gazeti la Anuur limeendeleza malumbano likisema kuwa hii ni sensa ya liwalo na liwe na kuwa serikali inasema sensa ipo hali waislamu wakisema hakuna kuhesabiwa.mwisho likahitimisha kuwa hii ni sensa ya liwalo na liwe
JK AMPA SHAVU DIAMOND PLATNUMZ IKULU
Stori: Sifael Paula RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemuita ikulu mwanamuziki anayefanya vizuri kwa sasa kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ na kumpa jukumu maalum, Ijumaa linairusha hewani. Kwa mujibu wa Diamond, juzikati ‘prezidenti’ alimwita ikulu Magogoni, Dar es Salaam na kumpa shavu la kwenda kufanya shoo kwenye mkutano maalum utakaofanyika Washington DC nchini Marekani hivi karibuni. “Yaa, rais aliniita akaniambia kuna shoo natakiwa kwenda kufanya Marekani. “Kwa mara ya kwanza nitasafiri nje ya nchi na madensa wangu wanne na msemaji mmoja. Sasa hivi hawataki kutembea na kupanda magari wasije wakakosa hiyo safari,” alisema Diamond na kuongeza kuwa baada ya kuumwa, mawazo aliyaweka kwenye mchongo huo hivyo mambo mengine yataendelea ikiwa ni pamoja na kufanya kolabo na mwanamuziki wa kimataifa wa Nigeria, J. Martins.
Thursday, 23 August 2012
HIVI KWELI TUNAWEZA KUTHUBUTU KUSEMA KWAMBA TANZANIA KUNA AMANI KWA MTINDO HUU?????
Baadhi ya wakazi wa eneo la wazi lililovamiwa na kumilikiwa isivyo halali na watu maeneo ya Madale, Kinondoni Dar es Salaam, ambako Polisi walikuwa wakiendesha oparesheni ya kuvunja nyumba na vibanda vyao, wakiwa wamewekwa kwenye gari tayari kupelekwa kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini.
Askari Polisi akiangalia mabaki ya kibanda kilichobomolewa na tingatinga la Manispaa ya kinondoni wakati wa zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi maeneo ya Madale, Kinondoni jijini Dar es Salaam juzi.
Askari Polisi akiangalia badhi ya vifaa vilivyokuwemo ndani ya moja ya kibanda kilichobomolewa na tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, wakati wa zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi maeneo ya Madale, Kinondoni jijini Dar es Salaam juzi.
Askari Polisi wakiangalia mabaki ya kibanda kilichobomolewa na tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, wakati walipokuwa wakisimamia zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi maeneo ya Madale, Kinondoni jijini Dar es Salaam juzi.
Askari Polisi, akimuongoza mmoja wa vijana waliokuwa wakiwatishia, wakati walipokuwa wakisimamia zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi maeneo ya wazi, Madale Kinondoni, jijini Dar es Salaam kuelekea kwenye gari tayari kwa kuwapeleka kituoni juzi.
Mmoja wa askari Polisi, akimuongoza kijana mwingine aliyekuwa akiwatishia, wakati walipokuwa wakisimamia zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi maeneo ya wazi, Madale Kinondoni, jijini Dar es Salaam kuelekea kwenye gari tayari kwa kuwapeleka kituoni juzi.
Askari Polisi wakiwa wamesimama sehemu kilipobomolewa moja ya vibanda juzi, vilivyojengwa kwenye sehemu za wazi zinazodaiwa kuvamiwa isivyo halali na watu ambao walikuwa wakiviuza kwa baadhi ya wananchi maeneo ya Madale, Kinondoni, Dar es Salaam.
Tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, likivunja moja ya vibanda vilivyojengwa kwenye eneo lililovamiwa maeneo ya Madale Kinondoni jijini Dar es Salaam juzi.
Dereva wa gari la Jambo Leo, Privatus Kachema, akiangalia zoezi la uvunjaji wa nyumba na vibanda vya wavamizi maeneo ya Madale Kinondoni, jijini Dar es Salaam juzi.
Moja ya nyumba zilizovunjwa katika oparesheni ya uvunjaji wa nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi la Madale juzi.
Tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, likivunja moja ya vibanda vilivyojengwa kwenye eneo hilo la wazi.
Tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, likiendelea kuvunja moja ya vibanda vilivyojengwa kwenye eneo.
Askari Polisi na Mgambo wa Manispaa ya Kinondoni, wakikagua moja ya kibanda kabla ya kuvunjwa na tingatinga la Manispaa hiyo, wakati wa zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi Madale Kinondoni, jijini Dar es Salaam juzi.
Askari Polisi na mgambo wa Manispaa ya Kinondoni wakiangalia tingatinga la Manispaa hiyo, wakati likivunja nyumba na vibanda vilivyojengwa kwenye sehemu za wazi zinazodaiwa kuvamiwa isivyo halali na watu ambao walikuwa wakiviuza kwa baadhi ya wananchi wengine maeneo ya Madale wilayani humo.
Askari Polisi wakiangalia mabaki ya kibanda kilichobomolewa na tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, wakati walipokuwa wakisimamia zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi maeneo ya Madale, Kinondoni jijini Dar es Salaam juzi.
Moja ya bango lililokutwa limeandikwa na watu hao, likiwa na ujumbe uliokuwa ukimshutumu Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela na OCD wake.
Mmoja wa watu wanaodaiwa kuwa wavamizi wa eneo hilo, aliyejitambulisha kwa jina la Hussein Said, akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kupata athari kichwani wakati alipokuwa akiwekwa chini ya ulinzi na askari Polisi kwenye maeneo hayo. Picha zote na Kassim Mbarouk wa Bayana Blog.
MRAMBA ADAI ASINGEWEZA KUKANUSHA MAAGIZO YA RAIS WA WAKATI HUO BENJAMIN WILLIAM MKAPA. AMTAJA BALALI KATIKA KESI YAKE
ALIYEKUWA Waziri wa Fedha katika Serikali ya Awamu ya Tatu, Basil Mramba, amesema kutokana na mkataba uliosainiwa na Gavana wa Benki Kuu (BoT), Dk. Daudi Balali na Kampuni ya Alex Stewart, hakuwa na njia yeyote ya kukwepa kuondoa kodi kwa kampuni hiyo.
Mramba pia aliieleza mahakama kuwa, alipokea barua iliyotoka kwa Katibu wa Rais Benjamin Mkapa kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na nakala iliyokwenda kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati huo, Andrew Chenge, ikiwataka kutafuta fedha za haraka kwa ajili ya kuilipa kampuni hiyo.
Hayo aliyaeleza jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, John Utumwa, wakati akitoa utetezi katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 11.7, inayomkabili yeye na wenzake wawili.
Mramba alieleza kuwa, mkataba uliotiwa saini kati ya BoT na kampuni hiyo ulikuwa unambana kwa mujibu wa sheria ya mkataba huo kwani asingetoa msahama wa kodi, serikali ilitakiwa kumlipa fedha nyingi mwekezaji huyo.
Akiongozwa na wakili wake, Hulbert Nyange, aliyetaka kujua kama maagizo hayo yote aliyachukuliaje kama Waziri wa Fedha, Mramba alidai kuwa yalitolewa na Rais Mkapa katika dokezo mbalimbali akitaka utekelezaji wa kuilipa kampuni hiyo ufanyike haraka iwezekanavyo.
“Mimi sikuruhusu malipo yoyote wala punguzo lolote ila kwa mujibu wa kifungu cha 4 (3), kinasema malipo yoyote hayatatozwa kodi kwa mujibu wa mkataba huo kati ya BoT na Kampuni ya Stewart,” alidai Mramba.
Wakili Nyange alitaka kujua kama ni kweli Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) walitoa ushauri kwa Wizara ya Fedha kuwa wasitoe msahama huo, ambapo alidai kwamba hakuuona ushauri huo.
Aliongeza kuwa yeye hakupaswa kupewa ushauri na TRA, bali kupewa na katibu wake ingawa alikiri kuwahi kuona barua kutoka TRA baadaye, japokuwa ilikuwa imechelewa kwa muda wa siku kumi wakati yeye akiwa ameshaondoa kodi kwa kampuni hiyo.
“TRA hata wangeshauri kwa mujibu wa maagizo niliyoyapata, ingekuwa kazi bure, kwanza walishachelewa. Na hata hivyo tangu kupata Uhuru, sheria inatoa mamlaka kwa waziri wa fedha kusamehe kodi ilimradi msahama huo uwe na manufaa kwa wananchi wake bila kushauriana na mtu yeyote,” alidai Mramba.
Alipoulizwa kuwa inadaiwa alikurupuka baada ya kulala nyumbani kwake na asubuhi akaandika dokezo kwa serikali la kuondoa kodi hiyo, Mramba alisema hakufanya hivyo bali Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliagiza kufanya hivyo na kwamba yeye alitekeleza maagizo hayo.
Mramba, Daniel Yona aliyekuwa Waziri wa Fedha na aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Grey Mgonja, walifikishwa mahakamani mwaka 2008 wakidaiwa kuwa kati ya Agosti 2002 na Juni 14, 2004, Dar es Salaam, washtakiwa wakiwa watumishi wa umma, walitumia vibaya madaraka yao na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 11.7.
Ilidaiwa kuwa washtakiwa hao waliipatia msamaha wa kodi isivyo halali, Kampuni ya M/S Alex Stewart ya Uingereza. Kesi hiyo imehairishwa hadi Oktoba 12 mwaka huu, ambapo Mramba ataendelea kutoa ushahidi wake mahakamani hapo.
Tanzania Daima
MWAKYEMBE AWAWAKIA BANDARI. AMSIMAMISHA MKURUGENZI MKUU WA BANDARI.
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatangazia waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana, juu ya kuwasimamisha kwa muda Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA) na Watendaji wengine wa Mamlaka hiyo ili kupisha uchungunzi wa tuhuma mbalimbali katika bandari. Picha na Fidelis Felix
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Ephraim Mgawe, wasaidizi wake wawili na Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Cassian Ng'amilo kupisha uchunguzi wa wizi wa vitu mbalimbali yakiwamo makontena 40 ya vitenge, katika Bandari ya Dar es Salaam. Dk Mwakyembe alitangaza uamuzi wake huo jana jijini Dar es Salaam, akiendeleza kile alichokifanya Juni 5 mwaka huu alipomtimua kazi aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi. Hata hivyo, waziri huyo hakutaja majina ya vigogo waliosimamishwa na badala yake alitaja nafasi walizokuwa wakizishikilia ambazo ni pamoja na Meneja wa Kituo cha Mafuta ya Ndege Kurasini (Kurasini Oil Jet - KOJ), Meneja wa Kituo cha Mafuta JET na mhandisi wa mafuta wa kituo hicho, baada ya kubainika kuwapo kwa wizi wa mafuta. Kutokana na uamuzi huo, Dk Mwakyembe amemteua Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira katika Wizara ya Ujenzi, Injinia Madeni Kipande kukaimu nafasi ya Mgawe. Gazeti hili lilimtafuta Mgawe kwa simu kuzungumzia uamuzi huo, lakini simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita muda wote bila majibu na wakati mwingine kukatwa. Uamuzi huo umekuja baada ya kuwapo kwa taarifa za kupotea kwa makontena takriban 40 ya vitenge na vitu mbalimbali, yaliyokuwa yakipelekwa nchi jirani. Dk Mwakyembe alisema ameunda kamati ya watu saba ambao hakuwataja majina ili kuchunguza wizi huo na kwamba amewapa wiki mbili tu, wawe wamekamilisha kazi hiyo. “Nimeunda kamati ya kuchunguza suala hili, nimewapa hadidu za rejea zenye maswali 50..., majina ya waliopo katika kamati hii siyatangazi kwa sasa kwa sababu zangu binafsi,” alisema Dk Mwakyembe. Alisema amechukua uamuzi huo baada ya kukutana na Bodi ya Wakurugenzi ya TPA juzi na kwamba hawezi kuvumilia kuona nchi inakosa mapato kwa sababu ya wizi uliokithiri. Alisema kwa muda mrefu katika bandari hiyo ya Dar es Salaam, kumekuwa na malalamiko ya wizi wa vitu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ule wa vifaa vya magari, mafuta na kukithiri rushwa. Alifafanua kwamba wizi huo umesababisha Bandari ya Dar es Salaam kukimbiwa na wateja ambao hivi sasa wanatumia bandari za Kenya, Msumbiji na Afrika Kusini. “Makontena yanaibwa kama njugu, hivi sasa watu wa Rwanda, Uganda DRC hawaitumii tena Bandari ya Dar es Salaam, wanaona bora waingie hasara na wameanza kupitisha mizigo yao katika Bandari ya Mombasa Kenya, Beira nchini Msumbiji na Durban Afrika Kusini,” alisema Dk Mwakyembe. Dk Mwakyembe alisema kuwa hivi karibuni mfanyabiashara mmoja mwanamke alitishia kuhamia nyumbani kwake, baada ya kuibiwa kontena zima la vitenge vilivyokuwa na thamani ya dola 180,000 za Marekani. “Ni mambo ya ajabu sana hatuwezi kuwa na maendeleo kwa masuala ya ‘kisanii’ kama haya, nimeamua hivi kutokana na mamlaka niliyonayo na uamuzi nitakaouchukua najua wenzangu watanielewa,” alisema. Wakati akieleza majukumu ya Mamlaka hiyo alisema, “Nimewataka TPA watambue majukumu yao jinsi yalivyo nyeti, nimewaeleza wazi kuwa imani ya wananchi imepungua sana kwa mamlaka hiyo. “Kama waziri mwenye dhamana sitakuwa tayari kuona jambo hili linaendelea, hili suala haliwezi kuachwa likaendelea ni lazima uchunguzi ufanyike.” Dk Mwakyembe alisema kuwa ameiagiza bodi ya wakurugenzi, kitengo cha sheria TPA kiuchambue upya mkataba wa Kampuni ya Kupakia na Kupakua Makontena katika Bandari ya Dar es Salaam (Ticts) na kumpatia taarifa Jumatano ijayo. “Kontena likiwa na vitenge hata ukiweka askari 40 linaondoka, tumepoteza wateja wengi na watu wanaona bora kukimbilia bandari nyingine, nimewaagiza wauchambue upya mkataba huu,” alisema Dk Mwakyembe. Agizo Alisema ili kukomesha rushwa ameitaka Bodi ya Wakurugenzi TPA, kuanzia Septemba mosi mwaka huu kuacha kutumia utaratibu wa kulipa fedha dirishani, badala yake fedha zote zilipwe kupitia benki. “Mtindo wa malipo ya fedha dirishani ndiyo unachochea wizi unaofanywa na mtandao wa kisanii pale TPA. Nimeagiza malipo yote yafanyike kupitia benki au kwa njia zozote za teknohama kuanzia Septemba mosi,” alisema Dk Mwakyembe na kuongeza: “Kama malipo haya yakiendelea mwezi ujao watakaolipa waandike tu wenyewe barua za kuacha kazi, kampuni ndogondogo nchini zinalipa fedha kupitia benki, kwa nini TPA washindwe?” Aliongeza kuwa ameiagiza bodi hiyo kuangalia upya mfumo mzima wa uongozi wa TPA na bandari kwa kuwa kuna viongozi wana mamlaka makubwa wakati vyeo vyao ni vidogo. “Meneja wa bandari ana mamlaka makubwa kiasi kwamba utendaji kazi ndani ya bandari unasuasua wakati wapo viongozi wa juu yake,” alisema Dk Mwakyembe. Wizi wa mafuta Akizungumzia wizi wa mafuta, Dk Mwakyembe alisema katika kituo cha KOJ kuna wizi mkubwa wa mafuta ambapo wahusika wakibanwa hutoa kisingizio kuwa mafuta yanayochukuliwa ni machafu. “Mafuta yale siyo machafu, hiyo imekuwa ndiyo biashara yao kila mwaka, ndiyo maana tenda ya mafuta machafu inagombewa sana, tumefuatilia na kugundua kuwa yanapelekwa katika vituo mbalimbali vya mafuta nchini” alisema Mwakyembe na kuongeza: “Niliwahi kwenda katika eneo lile saa 12 asubuhi na kukuta malori yanajaza mafuta. Niliuliza lori lina uwezo wa kupakia lita ngapi, kuanzia meneja mpaka watu wa chini kabisa walishindwa kunijibu.” Alisema kutokana na kitendo hicho, amechukua sampuli ya mafuta hayo na kuyapeleka Mombasa, Kenya kuyapima ili kugundua yana kiwango cha mafuta masafi kwa asilimia ngapi. Alisema kuwa malori hayo yana uwezo wa kupakia lita 26,000 za mafuta lakini wahusika wanadai kuwa yanaweza kupakia lita 9,000 tu. “Mafuta haya huibwa wakati yakitolewa katika meli na kupelekwa katika magari, karibu asilimia mbili nzima ya mafuta huibwa, kiwango ambacho ni kikubwa sana,” alisema. Alisema kutokana na hali hiyo ameagiza kurejeshwa kwa kifaa cha kupimia wingi wa mafuta katika malori ya mafuta, ndani ya mwezi mmoja kuanzia jana. Aanika ufisadi Alisema kampuni ya Singirimo iliyopewa zabuni ya kusafirisha mafuta machafu, mkataba wake ulishaisha siku nyingi, lakini bado inaendelea na kazi hiyo na kwamba mwaka 2008, Ikulu iliwahi kueleza kuwa kampuni hiyo ni kinara kwa kusafirisha mafuta masafi na kudai machafu. “Kampuni hii kila mwaka inashinda tenda ya kusafirisha mafuta tu, hivi sasa inachunguzwa na Ewura na Takukuru, nimeagiza mamlaka husika kwamba kampuni hii isijihusishe tena na usafirishaji wa mafuta ili kupisha uchunguzi,” alisema Dk Mwakyembe na kuongeza: “Kampuni iliyokuwa namba mbili katika utoaji wa tenda ndiyo ipewe jukumu hilo na kama isipopewa ndiyo nitajua kuna kitu kinaendelea.” Alisema kuwa mwaka 2008 Ikulu ilisema kuwa kampuni ya Singirimo ni ya wafanyakazi na vigogo wa TPA na inasafirisha mafuta masafi na kudai kuwa ni machafu Chanzo:Mwananchi.co.tz |
TASWIRA YA OPERESHENI SANGARA MVOMERO
Katibu Mkuu wa BAVICHA Deogratias Munishi akimkabidhi kadi ya CHADEMA aliyekuwa mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Kododo jimbo la Mvomero, bwana Charles Kiwaga. Wengine ni wanachama wapya wa CHADEMA tawi la Kododo Mvomero.
Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM kata ya Muhonda akieleza jinsi alivyokunwa na sera za CHADEMA zilizoelezwa na katibu Mkuu wa BAVICHA katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kichangani.
Mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Kododo, Charles Kiwaga (kulia) akifafanua kero ya shule ya msingi kododo kwa kayibu mkuu wa Bavicha Deogratias Munishi. Katikati ni mjumbe wa kamati ya maendeleo ya elimu ya shule hiyo. Shule hii ina wanafunzi 652 na mwalimu mmoja tu.
Na Mdau Hellen-Morogoro
Operesheni Sangara inayoendelea kwa upande wa Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), Bwana Deogratias Munishi amezidi naye kupasua vijiji ndani ya Mvomero, Morogoro. Pia wanavijiji walimuonyesha hali halisi ya maendeleo katika kata yao ya Luale kwa kipindi kirefu walichokuwa chini ya CCM tangu miaka 50 iliyopita mpaka sasa na wakiwa wamekata shauri kujiunga na CHADEMA kama chachu ya mabadiliko.
Chanzo:Mjengwa blog.com
NAIBU WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA HAILEMARIAN DESALEGN KUSHIKIRIA WADHIFA WA ALIYEKUWA WAZIRI MKUU MPAKA HAPO UCHAGUZI UTAKAPOFANYIKA
Mwili wa Wariri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi umelakiwa na maelfu ya watu waliokuwa wakilia wakati wa kipindi rasmi cha maombolezo kikianza baada ya kifo cha kiongozi huyo katika hospitali mjini Brussels.
Bendi ya jeshi ilipiga nyimbo za maombolezo wakati jeneza , lililofunikwa bendera ya taifa , likitolewa kutoka katika ndege ya shirika la ndege la Ethiopia tukio ambalo pia lilihudhuriwa na viongozi wa kisiasa , kidini na jeshi pamoja na wanadiplomasia.
Naibu waziri mkuu Hailemariam Desalegn, mwenye umri wa miaka 47, ambaye pia ni waziri wa Mambo ya Nje tangu mwaka 2010, ataongoza nchi hiyo kwa muda.
Vyombo vya habari vya taifa vimeripoti kuwa kiongozi huyo atabakia madarakani hadi uchaguzi wa mwaka 2015, licha ya kuwa huenda baadaye mwaka huu.
Meles Zenewi amefariki usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne kufuatia kuugua kwa muda mrefu.
This Day Magazine
MKURUGENZI MKUU WA BANDARI ASIMAMISHWA KAZI NA WAZIRI MWAKYEMBE

Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harisson Mwakyembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari-TPA-Ndugu Ephrahim Mgawe pamoja na wasaidizi wake wawili ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.
Wengine waliosimamishwa ni Meneja wa Mafuta ya Ndege Kurasini, Meneja wa JET na Meneja wa Oil Terminal kutokana na tuhuma za kupotea kwa mafuta na kuidanganya serikali kuhusu mafuta masafi na machafu.
Kutokana na kuwasimamisha kazi Wakurugenzi hao Dkt. Harisson Mwakyembe amemteua Injinia Madeni Kipange kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA.
Kufuatia tuhuma hizo zinazofanywa Bandarini Dkt. Mwakyembe ameunda Tume wa ya watu saba kufanya uchunguzi kwa wiki mbili na kumpelekea taarifa ofisini kwake ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo zikiwemo za wizi.
Pia ameagiaza kufikia Septemba Mosi mwaka huu malipo yote yafanyike benki ili kuondoa rushwa na wizi unaofanyika ndani ya Mamlaka hiyo.
Waziri Mwakyembe anachukua hatua hizo kutokana na wwadao wengi sasa hawaitumii Bandari ya Dar es salaam kupitisha mizigo yao kutokana na kutokuwa na inami na watumishi wake hatua inayoifanya serikali kukosa mapato.
Pia ameagiza kusimamishwa mara moja kwa Kampuni ya Singilimo ambayo inajihusisha na kazi ya kubeba mafuta machafu na badala yake itafutwe Kampuni nyingine.
JOB OPPORTUNITY WORLD VISION:Senior Legal Officer
World Vision Tanzania-Career
JOB OPPORTUNITY:Senior Legal Officer
Position Description:
Ref No WVT/P&C/F12/105
Job Title: Senior Legal Officer
Job Title: Senior Legal Officer
Reports to: People and Culture Director
Location: Arusha
Purpose of the position:
To support, coordinate and advise on legal matters affecting the organization to ensure compliance to various statutory requirement and serve as a vital link between the public and management on legal matters.
Major Responsibility:
Institute legal proceedings on behalf of the organization
Respond to correspondences and complaints with legal implication from WV partnership, Government and general public
Represent the organization in all judicial/quasi-judicial functions
Coordinates drafting and Vets all the contracts entered into between the organization and other parties
Asses legal risks and advise management on necessary amendments to the organization policies, rules and regulations
Coordinate the activities of external legal counsels and legal firms acting on behalf of the organization if any
Minimum Qualification required:LLB and should be registered to the High Court.
Experience: Four years as Advocate of the High Court
Preferred:Seven years of experience in the legal field
Technical Skills & Abilities:
Computer skills
Practice in Labour causes
Excellent communication skills both English and Kiswahili
Application Instructions:
Interested candidates who meet the above criteria should submit their updated CV before September 6, 2012 to wvt_recruit@wvi.org and copy to orestes_sotta@wvi.org. Please indicate the post you are applying as a subject matter
Location: Arusha
Purpose of the position:
To support, coordinate and advise on legal matters affecting the organization to ensure compliance to various statutory requirement and serve as a vital link between the public and management on legal matters.
Major Responsibility:
Institute legal proceedings on behalf of the organization
Respond to correspondences and complaints with legal implication from WV partnership, Government and general public
Represent the organization in all judicial/quasi-judicial functions
Coordinates drafting and Vets all the contracts entered into between the organization and other parties
Asses legal risks and advise management on necessary amendments to the organization policies, rules and regulations
Coordinate the activities of external legal counsels and legal firms acting on behalf of the organization if any
Minimum Qualification required:LLB and should be registered to the High Court.
Experience: Four years as Advocate of the High Court
Preferred:Seven years of experience in the legal field
Technical Skills & Abilities:
Computer skills
Practice in Labour causes
Excellent communication skills both English and Kiswahili
Application Instructions:
Interested candidates who meet the above criteria should submit their updated CV before September 6, 2012 to wvt_recruit@wvi.org and copy to orestes_sotta@wvi.org. Please indicate the post you are applying as a subject matter
TAASISI ZA KIDINI ZAKANUSHA UWEPO WA UAMSHO
Na: Idara ya Habari,MAELEZO
Taasisi mbalimbali za kidini hapa nchini zilizopata usajili rasmi kwa Mrajis Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimekanusha kuhusika na tamko lililotolewa na Amiri Mkuu wa Jumuiya ya Uamsho, Sheikh Mselem Ali la Waislamu wa Zanzibar wagomee kushiriki katika Sensa ya Watu na Makaazi Kitaifa inayotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo.
Wakizungumza na Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga Wawakilishi wa Taasisi hizo wamelaani tabia ya Uamsho ya kujipa Mamlaka ya kuzisemea Taasisi hizo.
Aidha,wameitaka Jumuiya ya Uamsho kuthibitisha ni kikao gani kilichokaa na kuzungumza na Taasisi za Kidini na kuamua kwa pamoja kutowa tamko hilo la kupinga kushiriki kwa Waislamu katika Sensa.
Aidha, wameihakikishia Afisi ya Mufti na Serikali kuwa watashiriki katika Sensa ili kusaidia maendeleo ya Zanzibar na kutatua baadhi ya migogoro ya kijamii na sio kujiingiza katika siasa na kupingana na Serikali kama ambavyo imekuwa ikifanya Jumuiya ya Uamsho.
Taasisi zimewataka Waislamu kushirikiana na Serikali na kuachana upotoshaji unaofanywa na Uamsho.
Aidha, wameitaka Jumuiya ya Uamsho kuachana mara moja kutumia kivuli cha umoja wa Taasisi za kidini Zanzibar wanapoamua mambo yao kwani Jumuiya hizo nyingi hazikubaliani na Sera yao ya fujo na vurugu.
Mwisho.
Imetolewa na:
Idara ya Habari(MAELEZO) Zanzibar
23/08/2012
HERE ARE TEN REASONS WHY WOMEN WILL GO BACK TO CHEATERS
Her love of winning not only creeps up in the boardroom, but in her relationship too. She hates the idea of falling short of a happy relationship or admitting defeat when it comes to love. So, she will try to work at the relationship — perhaps seeking counseling is an option — to ensure that the tear in the relationship gets stitched up. If her relationship were the Titanic, she’d be playing the violin till the last minute.
No.9 She’s afraid of the unknown
She’s been with him for years, building a life together and focusing on their combined futures. Thinking about letting all that go makes her queasy with fear of the unknown. She’s probably harried by concerns such as what her life will be like without him in it. Facing that uncertainty is often too scary of a prospect. She’d rather stick with the status quo because, as difficult as it might be, it’s a comfort zone.
No.8 She’s convinced he will change
Her boyfriend betrayed her, but she believes that he will change. In the stress of infidelity, many women feel that they don’t know how to piece together the image of the cheating boyfriend with the guy who used to shower them with affection and love. So they think it’s possible their boyfriends will change their cheating ways and revert to how they were before the infidelity. Of course, the relationship might have changed irrevocably, and not for their benefit.
No.7 She has low self-esteem
Brenda Stone Browder, author of On the Up and Up: A Survival Guide for Women Living with Men on the Down Low, who has also been on the receiving side of betrayal in relationships, says that women who don’t love or value themselves catch the cheater’s eye. If a woman doesn’t care about her self-worth, she’ll be quick to brush away his indiscretions, make excuses for him, and she won’t feel that she is wonderful enough to do better than him.
No.6 She’s possessive of him
Although he has hurt her deeply, she just can’t imagine being without him. But more than this, she cringes at the thought of another woman getting to have him. It might not make sense to you; you might think, “What would she want with a cheat, anyway?” but she’s so used to saying that he belongs to her, that she’s not quite ready to turn him into recycled goods for other women to enjoy. Staying with him is her way of marking — and keeping — her territory.
No.5 She has kids with him
Although it sounds naive, staying with a man for the children makes sense to the woman in question. As a mother, she has people other than herself to consider, and she might hesitate at the idea of breaking up the family by leaving her boyfriend or husband.
No.4 She has a history with him
Sharing past experiences is a powerful thing, especially for women who are known to be more sentimental. If her boyfriend is a large part of her past, she could be dragging her feet to leave because it means throwing away the construction of her relationship to date — in exchange for memories that won’t keep her warm at night.
No.3 She’s financially dependent on him
Emotions aside, not having money can cause a woman to stay in Cheat Street. How is she going to leave and start a new life on her own if she has been depending on him for financial stability? This is an issue that could keep women, both gold diggers and non- gold diggers alike, in the relationship — even if they’re not in love with their partners anymore.
No.2 She’s invested time and money
Building a relationship with someone is more than forging emotional ties; it can incorporate other financial, energy and time costs. For instance, if she has built a business with her guy, leaving the relationship could risk her venture. Likewise, having invested feelings and energy cultivating the relationship could make her hesitant to walk away with nothing. She would rather work on the current relationship than cut her losses.
No.1 She’s crazy in love
One of the most common things women say when they’re asked why they’re still in their betrayal-adorned relationship is, “But I love him.” Yes, she’s hurt and scalded by his actions, but she can’t deny that her strong feelings for him are causing her to plant her flag in the relationship and try to make things work, with Victoria Beckham as her new inspiration.
Source: This Day Magazine
Subscribe to:
Posts (Atom)

























