Subscribe:

search

.

Tuesday 14 August 2012

HAYA HAPA MAGARI YENYE UWEZO WA KUPAA NA KUTEMBEA NCHIKAVU PIA



 Hili ni Moja ya Magari hayo ambalo likitua tuu hapa linakuwa gari la kawaida 
 Hili lipo hapa linakaribia kuondoka 
 Hapa Gari Hilo likiwa Juu linakula mitaa
 Muda mchache baada ya kutua sasa lipo mtaani linatembea, 
 Foleni Ikizidi Hiloo lina tambaa juu 
 Hii ni Aina nyengine ya Magari hayo ambayo hupaa na kutembea nchi kavu
 Cheki Hapa limetua kwa kasi mwendo Mdundo linaendelea na safari 


 Hili ni aina ya Gari ambalo pia Hupaa na kutembea Barabarani
Hapa Kabla halija ondoka , Limekula pozi
Hapa linakula Kona.
Picha na Terrafugia
na Fredy Tony Njeje wa This Day magazine
***
Kutokana na kukuwa wa mabadiriko ya Science na Technology kumekuwa na mambo mengi sana ambayo yanatokea, lakini kubwa kabisa la siku ya leo ni ujio wa haya magari ambayo wanasayansi wanatarajia kuyazindua hivi karibuni, mpaka sasa yapo katika majaribio kabla ya kuanza kutumika Rasmi.

Wazo hili la kutengeneza magari haya yenye uwezo wa kutembea katika barabara za kawaida na kupaa angani limekuja kutoka Holy hood, ambapo wanasayansi hao walifanya utafiti kwa lengo la kutengeneza magari haya kama Taxii za mwendo kasi  ili kurahisisha safari za abiria wenye haraka zao, Lakini kwa mara ya kwanza mpango huo ulikwama kutokana na kwamba walikuwa hawajajiandaa, waliweka zaidi kama mpango wa kusadikika.

Baada ya  ya muda kupita waliweza kufanikiwa na mpango huo wa magari ambayo yanaweza kupaa angani endapo tuu kutakuwa na foleni kubwa hasa kwa nchi za Ulaya na Marekani.  
Kwa hakika magari hayo ambayo ni Technology mpya kabisa Hapa duniani ni ya kipekee na ambayo itawafanya watu wapate kuishi kwa amani kabisa. Akizungumza mmoja wa wagunduzi wa Magari hayo yaliyo pewa jina la "SKYWORTHY" amesema kuwa " Tumelazimika kutafuta ufumbuzi wa kupunguza msongamano wa foleni na kuwasaidia wenye haraka pindi wakiwa na haraka waweze kupaa moja kwa moja na kuwahi mambo yao"

Pia katika haya magari jambo la kufurahisha zaidi ni kwamba mbawa zake zimetengenezwa kiasi kwamba huwezi kuziona wakati Gari lipo barabarani, lakini wakati linaanza kupaa ndipo mbawa hizo zinatokezea, hilo ni swala ambalo wanasayansi hao wameonesha ubunifu mkubwa sana  na wakipekee, swala ambalo halijawahi kutokea hapo mwanzo.

Magari hayo ambayo pia ni Ndege yanatarajiwa kuzinduliwa mwaka huu 2012 ambapo gari la kwanza litauzwa kwa Gharama ya Dola za Kimarekani 300,000, ambapo ndege hiyo itakuwa na uwezo wa kupaa kwa masaa 20 angani.

Magari hayo ambayo pia ni ndege hapo hapo yana muundo wa Chopa , lakini ni ndogo zaidi ya Chopa, ina uwezo wa kukimbia (110mph/180 km/h) ambayo ni sawa na (560km/350Miles)

Usikose Siku nyengine tena katika Technology na This Day Magazine ambapo tutawaletea mambo mbali mbali na Mchambuzi wetu Fredy Tony Njeje.
www.thisdaymag.blogspot.com

0 comments: