Subscribe:

search

.

Friday 10 August 2012

MASTAA WA KIKE WASHUTUMIWA KUJIUZA KUPITIA BBM


BAADHI ya mastaa Bongo wanadaiwa kuwa na tabia ya kutumia mtandao wa simu wa BlackBerry Messenger ‘BBM’ vibaya ikiwa ni pamoja na kujiuza kwa wanaume, Ijumaa limebaini.
Utafiti uliofanywa na mapaparazi wetu umeonesha kuwa, wapo ambao wawapo vyumbani kwao hujipiga picha za utupu na kuzitupia kwenye mtandao huo kisha baada ya muda huzitoa.
Wakizungumzia tabia hiyo, baadhi ya wanaume wanaotumia BBM walikiri kukumbana na picha hizo za ajabu za mastaa huku zikiambatana na maneno ya kujitongozesha kwao.
“Huyu …(anataja jina la staa maarufu Bongo), juzi usiku mishale ya saa nane alianza kunitumia ‘sms’ kuniuliza kama niko macho. Nilipomjibu akaniambia kuna zawadi anataka kunipa, nilivyomkubalia akatupia picha yake akiwa kitandani mtupu.
“Hazikupita hata sekunde nyingi, kabla ‘sijai-download’ akaitoa kisha akaniuliza nimejisikiaje kumuona alivyo. Nilishangaa lakini nikamjibu kwa kifupi kuwa ana mvuto, basi kuanzia siku hiyo akawa ameniganda,” anasema kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Sule ambaye ni mfanyabiashara jijini Dar.
 Msanii mwingine wa kiume aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema:
“Mbona huo ndiyo mchezo wao, yaani ukishamkubalia kuwa rafiki yao basi subiri vituko, kwa kifupi sasa hivi wengi wanajiuza kupitia BBM.”
Katika kupata ukweli juu ya habari hiyo, waandishi wetu walizungumza na baadhi ya mastaa wa Kibongo wanaotumia mtandao huo ambapo walikuwa na haya ya kusema:

JACQUELINE PATRICK
Modo huyo mwenye jina kubwa Bongo alifunguka: “Kwa upande wangu siwezi kukataa kuwa sijawahi kuweka picha kama hizo, mimi ni mpenzi sana wa picha na ninaupenda sana mwili wangu hivyo nikipiga picha ya aina yoyote  lazima niitupie kwani ‘fansi’ wangu ndiyo wanaoweza kuniambia kama nimenenepa au nimekonda au kunisifia
“Suala la kutongoza wanaume naweza nikasema kuwa mimi siweki kwa sababu hiyo kwani marafiki zangu wote kwenye BBM wana wapenzi wao.” 

ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE’
Mwigizaji huyo ambaye pia ni mwanamuziki alisema: “Mimi sijawahi kumtongoza mwanaume na siwezi kwa sababu mila za kwetu zinasema mwanaume ndiye anatakiwa kumtongoza mwanamke hivyo mwanamke anayemtongoza mwanaume anakosea kwani ataonekana wa bei rahisi sana.
Labda wenzangu wanaweza kufanya hivyo kupitia njia hiyo.”

MIRIAM JOLWA ‘JINI KABULA’
Mwigizaji huyo alifunguka: “Mimi nina mume wangu, nampenda sana na mara nyingi siingii BBM ila ninauzisha tu picha zangu kule lakini kuchati na watu siyo kivile na siwezi kumtongoza mwanaume kwa sababu wanaume wanaopatikana kwa njia hiyo siyo kabisa labda mastaa wenzangu, lakini mimi sijawahi kumtongoza mwanaume.”

RACHEL HAULE ‘RECHO’
Staa huyo wa filamu alisema: “Sijawahi kumtongoza mwanaume ila suala la kutongozwa na wanaume kwenye BBM ni la kawaida, inategemea na msimamo wa mtu. Najua BBM tumejiunga kwa ajili ya kujua matukio yanayotokea kwa haraka zaidi na siyo kwa ajili ya kujiuza.”

ISABELA MPANDA
Mwigizaji huyo alitiririka: “Katika orodha ya hao wanaojiuza kupitia mtandano huo, mimi simo. Nipo BBM ila sijawahi kumtongoza mtu wala kutupia za utupu.”
RUTH SUKA ‘MAINDA’
Mwigizaji huyo mkongwe alisema: “Ni kweli nimejiunga BBM lakini kwa sasa nipo ‘shouting’ nicheki baadaye.
Mastaa wengine waliotajwa kuwepo BBM nja na waigizaji Aunt Ezekiel, Irene Uwoya, Agnes Gerard ‘Masogange’ na wengineo.
Chanzo;www.globalpublishers.info

0 comments: