search

.

Tuesday, 2 October 2012

AJALI MBAYA YA ROLI LA MAFUTA ILIYOTOKEA MBALIZI MBEYA HII HAPA Na: Charles Mwaipopo wa MALAFYALELEO-Blog, Mbeya. 

Macho ya mwandishi wa habari hii ameshuhudia miili tisa ikiwa imeungua vibaya na kutawanyika baada ya lori lililokuwa na mafuta linalosadikiwa ni mali ya kampuni la LAKE OIL lenye namba za usajili T 814 BTC lililokuwa na tera ambalo namba zake ahazitambulika mara moja kufuatia kuungua vibaya. Mwandishi wa habari hii anasema ajali hiyo imehusisha magari matatu, Lori lililokuwa na namba za usajili T 299 BCE lililokuwa likishuka taratibu mteremko wa Mbalizi. 

Pia Hiace T 887 AHT linalofanya safari zake Mbalizi na Mwanjelwa na Gari Ford Double Kibbin linasadikiwa kumilikiwa na Mbunge wa Viti maalum kwa tiket ya Chama cha Mapinduzi, Mary Mwanjelwa ambalo namba zake hazikupatikana mara moja kutokana na kuungua vibaya. Shuhuda wa ajali hiyo aliyefahamika kwa jina la Sadiki Nurdin ambaye ni utingo wa Lori lenye namba T 299 BCE amemwambia mwandishi wa habari hii kwamba lori lilikuwa na mafuta likiwa nyuma yao aliliona likija kwa mwendo kasi hivyo alimshtua dereva wake na hivyo kulikwepa. 

Utingo huyo ameongeza kusema walipolikwepa lilianza kula ubavu wa gari lao na hatimaye lilikwenda na kukutana uso kwa uso na Hiace pamoja na gari linalosadikiwa ni la Mbunge wa Viti Maalum CCM na kusababisha maafa hayo. Mwandishi wa habari hii amesema kwa haraka haraka waliokufa ni 9, wawili kutoka kwenye Lori ambalo limelipuka na kusababisha maafa hayo, watu 6 kutoka kwenye basi la abiria aina ya HIACE, mpanda baiskeli, na mwendesha bodaboda. 

 Mwandishi wa habari hii anasema idadio ya majeruhi hajipata bado licha ya kwamba wamefikishwa katika hospitali ya Ifisi Mbeya Vijijini. Zoezi la uokoaji kwa mara ya kwanza limefanywa na Koplo Mathias Joachim wa Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania 44 KJ Mbalizi Mbeya. Mashuhuda wa tukio hilo wampongeza sana Koplo huyo kwani ndiye aliyeweza pekee kuingia katika moto uliokuwa ukiwaka kwa nguvu katika ajali hiyo.

Chanzo:Mjengwablogsport.com

0 comments: