Subscribe:

search

.

Tuesday 21 August 2012

LINDI WAASWA

Halmashauri za Wilaya Na Manispaa katika Mkoa wa Lindi zimetakiwa
kutenga bajeti ya kutosha ya kuhudumia michezo hasa ujenzi wa viwanja
vya michezo ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa viwanja hivyo.

Akifunga rasmi mashindano ya Imran cup yaliyomalizika jana na
kushirikisha timu 7 za Manispaa ya Lindi,Mkuu wa Mkoa wa
Lindi,Ludovick Mwananzila alizitaka Halmashauri hizo kuthamini Michezo
ikiwa pamoja na utengaji na Ujenzi wa Viwanja vya Michezo ili kuibua
vipaji vya Wanamichezo

Ili kuinua sekta ya michezo katika ngazi yoyote kama hutakuwa na
viwanja vya kutosha na vilivyo katika ubora unaostahili kwa michezo
husika. Ikiwa pamoja na uwepo wa ufinyu wa bajeti ya michezo

‘’Wakurugenzi kupitia maafisa michezo nawaomba kupanga bajeti za
michezo na pia lazima mtenge maeneo ya viwanja na huu wa Ilulu
uboreshwe kwa kuwa ndio kioo cha Mkoa katika viwanja;;;Alisisitiza
Mwananzila

Awali akitoa taarifa ya Mashindano hayo kwa Mgeni rasmi,Mratibu wa
Mashindano hayo ambae pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa
Habari Mkoa wa Lindi,Abdulaziz Ahmeid alimuomba mkuu wa Mkoa wa Lindi
kuangalia Uwezekano wa kuunda Mfuko wa kusaidia Michezo Lindi kwa
kuchangisha kupitia Mazao,Mafuta na Vinywaji ikiwa Pamoja na Kuona
umuhimu wa kutenga maeneo ya Ujenzi wa Viwanja

Katika Fainali hiyo Timu ya Lunduno Fc Ya Kata ya Mikumbi iliibuka
kidedea na kutwaa kikombe cha Ligi hiyo pamoja na seti ya jezi baada
ya Kuifunga Timu ya Kata ya Nachingwea .Manispaa ya Lindi kwa mabao 6
kwa 5 baada ya kupigiana Mikwaju ya penalty baada ya Kumalizika kwa
dakika 90 mabao yakiwa bila kwa bila
Timu zilizoshiriki ligi hiyo ni Nachingwea fc,Brazil Fc,Makavu
Fc,Kusini Soccer,Lunduno sc,Mtanda Fc na Lindi Sports zote toka
Manispaa ya Lindi

Fainali za ligi iliyokuwa katika sikukuu za Idd el fitr ziliendana na
michezo ya kukimbia,kufukuza kuku,kukimbia na magunia pamoja na mbio
za baiskeli kuzunguka uwanja wa Ilulu

0 comments: