search

.

Monday, 13 August 2012

MBOWE ADAI HAONGOZI GENGE LA WATU WANAOSAKA UONGOZIMwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Freemaan Mbowe amesema kamwe haongozi kundi au genge la wasaka vyeo na madaraka ndani ya chama chake bali anaongoza kundi la watu wanaopenda mabadiliko.Kiongozi huyo amesema binafsi hawezi kwa sasa kusema atagombea Urais au Ubunge kwa sababu huu si muda wake hata kidogo.

Mbowe amesema mwanachama yeyote makini wa Chadema kwa sasa ni muda wa kuwaunganisha wanachama na watanzania kwa ujumla na wala si muda wa kuwagawa kukimbilia madaraka. Kiongozi huyo amesema ndiyo maana makamanda wote wakiongozwa na Dr Slaa wamejichimbia vijijini kwa kazi moja tu ya kueneza vuguvugu la mabadiliko-M4C.

Chanzo: Tanzania Daima.

0 comments: