search

.

Monday, 13 August 2012

OLIMPIKI YAMALIZIKA, TANZANIA YAONDOKA BILA MEDALI YOYOTE KWA MWAKA WA 32 MFULULIZO.


Na: Imani Makongoro
NDOTO za Tanzania kutwaa medali kwenye michezo ya Olimpiki zimeendelea kuyeyuka baada ya jana, mwogeleaji mwingine, Magdalena Moshi kushindwa kufurukuta.

Magdalena ameshindwa kupenya katika mchujo wa mita 100, free style hatua ya makundi baada ya kutumia muda wa dakika 1:05:80.

Magdalena anakuwa mchezaji wa tatu wa Tanzania kuondolewa katika hatua za awali za michezo hiyo inayofanyika London, England.

Wengine waliong'olewa mapema ni bondia Seleman Kidunda na mwogeleaji Ammaar Ghadiyali.
Tegemeo pekee la Tanzania kwenye Olimpiki sasa limebaki kwa wanariadha Mohamed Msenduki, Faustin Mussa na Samson Ramadhan.
Chanzo:This Day Magazine

0 comments: