search

.

Saturday, 13 October 2012

BINGWA WA KULA MENDE AFARIKI GHAFLA


Jamaa mmoja huko Florida Kusini Edward Archbold mwenye umri wa miaka 32 ameanguka ghafla  na kufariki muda mfupi baada ya kuibuka bingwa katika shindano la kula dazeni kadhaa za mende walio hai.
Takriban washiriki 30 walishindana kula mende na wadudu katika kinyang’anyiro hicho kilichofanyika Ben Siegel Reptile Store huko Deerfield Beach umbalo wa kilometa 40 Kaskazini mwa Miami.

Mamlaka za eneo hilo zinasubiri uchunguzi mwili wa bingwa huyo ili kuweza kujua nini hasa sababu ya kifo chake.
Hata washindani wengine hakuna aliyeugua wala kupata matatizo yeyote.
Akizungumzia kuhusu kula mende, Profesa wa entimologiwa wa Chuo Kikuu cha California Michael Adams amesema kula mende hakuwezi kuleta madha yeyote mwili labda kama mende hao wamesibikwa na sumu.
Cha kushangaza ni kwamba zawadi ya mshindi wa kwanza ilikuwa nyoka aina ya Chatu.


0 comments: