search

.

Wednesday, 3 October 2012

BREAKING NEWS: BWENI LA CHUO CHA KILIMO NALIENDELE-MTWARA LATEKETEA KWA MOTOHabari za kusikitisha  zimelifikia dawati letu la habari hivi punde kuhusu kuungua kwa  baadhi ya Majengo ya Chuo cha Kilimo cha Naliendele Mtwara. Mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho amesema kuwa  hadi sasa moto bado unaendelea ila Wafanyakazi wa zima moto wa Bandari na Airport wamefika eneo la tukio ingawa wamechelewa kufika kwa saa moja zaidi, Mwanafunzi huyo amesema  hadi sasa ni bweni la Wasichana tu ndio lililoathirika. Chanzo cha moto huo hakijafahamika  hadi sasa,  na tumeshindwa kujua kama kuna  majeruhi  au ni  hasara ya kiasi gani imetokea.
 
Endelea kufuatilia blog hii kwa taarifa zaidi. 
Chanzo: Afrokija

0 comments: