search

.

Wednesday, 3 October 2012

HIVI NDIVYO HALI ILIVYOKUWA KATI YA YANGA NA SIMBA. MCHEZO ULIISHA KWA KUTOSHANA NGUVU SIMBA 1 YANGA 1Mchezaji Simon Msuva wa Yanga akikokota mpira mbelea ya mchezaji Christopher Edward wwa Simba  katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliokutanisha timu mbili za Simba na Yanga ambazo ni watati wa jadi kwenye uwanja wa Taifa usiku huu jijini Dar es salaam mpira umekwisha timu zote zimetoka sare ya  magoli 1-1 goli la Simba limefungwa na mchezaji Amri Kiemba katika dakika ya tatu ya mchezo huo na goli la Yanga limefungwa kwa njia ya penati na mchezaji Said Bahanuzi baada ya Felix Sunzu wa Simba kuunawa mpira katika eneo la hatari
Mashabiki wa timu ya Yanga walikuwa na hamu ya angalau kurudisha magoli 5 waliyofuwngwa na watani wao Simba hata hivyo wamefanikiwa kutoka sare na kutoshana nguvu katika mchezo huo
Mchezaji wa Yanga Mbuyu Twite kushoto na Christopher Edward wa Simba wakiruka juu kuwania mpira haupo pichani katika mchezo wao wa ligi kuu uliofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa usiku huu
Wachezaji wa timu ya Simba wakishangilia goli mara baada ya kuifunga Yanga katika dakika ya tatu kipindi cha kwanza.
Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia kwa nguvu wakati timu yao ikimenyana na timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam kwenye uwanja wa Taifa usiku huu.

0 comments: