search

.

Friday, 5 October 2012

JK AKIWA ZIARANI CANADA


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada ya kupokelewa katika Bunge la Seneti la Canada. Kulia ni Spika wa Bunge hilo Mhe Noel Kinsella, anayefuatiwa na Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper na Spika wa Bunge la wawakilishi la Canada (House of Commons), Mhe Andrew Scheer pamoja na viongozi wengine wa bunge hilo Alhamisi Oktoba 4, 2012 

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi toka kwa Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo, Alhamisi Oktoba 4, 2012

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Spika wa Bunge la Seneti la Canada  ramani ya dunia na njia za meli, pamoja na kuoneshwa chemba ya mikutano ya Maseneta wa Bunge la Canada  Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper wakitembea kuelekea kwenye chumba cha mkutano kuongea na wanahabari. Zuria jekundu na bendera za Canada za kiongozi wa  nchi husika huwekwa sehemu hiyo kwa heshima na wakati wa ziara ya kiongozi wa nchi ya nje aliye katika ziara rasmi nchini humo
Picha na IKULU

0 comments: