Subscribe:

search

.

Wednesday 17 October 2012

KIFO CHA KAMANDA BARLOW MWILI WAAGWA

 Mwili wa aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow umeangwa leo jijiniDar Es Salaamtayari kwa kupelekwa mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.
Katika shughuli hiyo Jeshi la polisi limeahidi kuwasaka wahusika walioshiriki katika tukio la kuuawa kwake na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema wakati wa sala ya kumuaga iliyofanyika katika kanisa katoliki la Ukonga jijini Dar es Salaam.
Shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama ambavyo vimepata nafasi ya kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu.
IGP Said Mwema alisema juhudi za kuwasaka watu walioshiriki tukiohilozinaendelea vizuri na hivyo wananchi wanahitaji kutoa ushirikiano ili kufanikisha suala ambalo linaonekana kurudisha nyuma kazi ya jeshi la Polisi.
Naye paroko msaidizi wa parokia ya Hananasifu Padre Veri Urio alisema hakuna mtu mwenye mamlaka ya kutoa uhai wa mwenzake hivyo lazima kila mtu awe na jukumu la kulinda uhai wake na wa watu wengine.
Marehemu Kamanda Barlow alizaliwa katika kijiji cha Kyou wilaya ya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro mwaka 1959 ambapo mwaka 1982 alijiunga na chuo cha mafunzo cha polisi CCP kwa ajili ya kusomea mafunzo ya awali ya sheria ya uhamiaji na baadaye kupangiwa katika mkoa wa Mtwara akiwa kama mkuu wa kituo.
Mwaka 2008 Barlow aliteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara kabla ya kuteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tabora mwaka 2010 nafasi aliyoshikilia hadi mwaka 2011 alipoteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza hadi mauti yalipomfika ambapo ametumikia jeshi kwa miaka 24.

0 comments: