Subscribe:

search

.

Friday 12 October 2012

MRADI WA MAJI KUTEKELEZWA MUSOMA

HATIMAYE Serikali imepanga kutekeleza mradi mkubwa wa maji katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara ambao unatarajia kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 41. Naibu waziri wa Maji Mh Mhandisi Dk Benilith Mahenge,ametoa taarifa hiyo mjini Musoma wakati akizungumza na uongozi wa mkoa wa Mara,ambapo amesema tayari mipango wa kuanza utekelezaji wa mradi huo mkubwa imekamilika baada ya serikali kupata fedha kutoka nchi za Ujerumani na Ufaransa.
Amesema mradi huo pamoja na kuchelewa kuanza utekelezaji wake kwa zaidi ya miaka mitatu lakini utalenga kuhamisha chanzo cha maji cha sasa na kujengwa upya katika eneo la Bukanga pamoja na kufufua na kuongeza miundombinu mipya ya maji ili kukidhi hitaji la maji kwa wananchi na taasisi zote katika Manispaa ya Musoma.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mara Bw John Tupa,pamoja na kupongeza hatua hiyo ya serikali kwa kukubali kutekeleza mradi huo katika unaolenga kuwandolea kero kubwa ya upungufu wa maji inayowakabili wananchi lakini pia ameahidi kuwa serikali ya mkoa itahakikisha inapambana na vitendo vyote vya hujuma ambayo inaweza kujitokeza katika utekelezaji wa mradi huo.

Wakati huo huo baadhi ya watumishi wa serikali katika mradi wa maji wa Mugango,Kiabakari hadi Butiama wanadai mishahara yao ya kati ya miezi 26 hadi 30 jambo ambalo limewafanya kuishi maisha ya kuomba omba. Wafanyakazi hao wametoa kilio hicho baada ya naibu waziri wa Maji Mh Mhandisi Dk Binilith Mahenge kutembelea mradi huo ambao pia umekuwa ukikabiliwa na uchakavu mkubwa wa miundombinu ya kusambazia maji kenda kwa wananchi ikiwemo familia ya baba wa Taifa hayati Mwl Julius Nyerere.
Wakiwa na mabango wafanyakazi hao ambao wengi ni vibarua wa kudumu wamemueleza na naibu waziri huyo kwa nyakati tofauti kuwa hivi sasa baada ya kutoka kazini wanalazimika kufanya vibarua vikiwemo vya kulima mashamba kwaajili ya kupata fedha za kuhudumia familia zao. Kufuatia kilio hicho,naibu waziri huyo wa maji,ameuagiza uongozi wa mamlaka ya maji ya Mugango,Kibakari hadi Butiama,halmashauri ya Musoma na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Butiama kumpatia maelezo ya sababu za wafanyakazi hao kutolipwa mishahara yao kwa kipindi hicho pamoja na kuorodhesha madai yote ambayo yanadaiwa na watumishi hao ndani ya siku tatu.

Amesema kushindwa kulipa mishahara hiyo kwa wakati kunaweza kuchangia watumishi wasio waaminifu kufanya hujuma kubwa ikiwa ni pamoja na kuiba mashine za mradi huo jambo ambalo linaweza kuingizia hasara kubwa serikali huku akitoa mwezi mmoja kwa meneja wa mradi huo mhandisi Merchedes Tibita kuongeza ukusanyaji wa mapato ambayo yatawezesha kutatua baadhi ya changamoto zinazoukabili mradi huo.

1 comments: