search

.

Tuesday, 9 October 2012

TUME YAWATAKA WATANZANIA KUJITOKEZA

 
Tume ya mabadiliko ya katiba imesema imeridhishwa na hatua iliyofikiwa katika mchakato mzima za ukusanyaji maoni.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Tume hiyo Mh. Jaji Joseph Sinde Warioba amesema wananchi wengi wameendelea kujitokeza katika mikutano ambayo Tume imekuwa ikiitisha katika maeneo mbalimbali ya nchi na wanatoa maoni kwa wingi.
Amesema hadi sasa Tume imetembelea mikoa 15 ambapo jumla ya mikutano 842 imefanyika na wananchi 517,427 wamehudhuria.

0 comments: