Subscribe:

search

.

Tuesday 21 August 2012

FFU WATUMIA MABOMU KUTAWANYA WANANCHI IRINGA



Askari wa FFU Iringa wakiwa wamemwokoa askari mwezao na mtuhumiwa wa wizi wa simu ambao walikuwa wamezungukwa na wananchi kwa ajili ya kuuwawa
Askari wa FFU wakimsaidia askari mwezao aliyevalia jezi nyekundu na mtuhumiwa wa wizi wa simu kuingia katika gari ya polisi huku ,hewani kukiwa kumetanda moshi uliotokana na mabomu ya machozi yaliyopigwa eneo hilo kuwatawanya wananchi ambao walitaka kufanya mauwaji dhidi ya askari huyo na mtuhumiwa wa wizi
Askari wa FFU wakifika eneo la tukio kumuokoa mwenzao na mtuhumiwa mmoja wa wizi wa simu wasiuwawa na wananchi
Askari aliyenusurika kifo akiwasiliana na jamaa zake kwa simu huku akilindwa na askari wa FFU
Wananchi wenye hasira kali wakimpiga askari huyo (mwenye T-Shert nyekudu ) ambaye alifika kusaidia kuokoa maisha ya mtuhumiwa wa wizi na kugeuziwa kibao

Askari huyo baada ya kuokolewa mikononi mwa wananchi 

ASKARI wa kutuliza ghasia (FFU) Iringa leo wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi zaidi ya 200 eneo la Kihesa mjini Iringa ambao walikuwa wakitaka kumuua kwa mapanga askari kanzu mmoja ambaye alifika kumwokoa kijana aliyefahamika kwa jinala Mtega aliyekuwa akituhumiwa kuiba simu.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa 2 mchana katika eneo la Kihesa Sokoni ambapo wananchi hao zaidi ya 200 wakiwa na silaha mbali mbali walianza kumshambulia mtuhumiwa huyo wa wizi wa simu pamoja na askari aliyefika kuwasihi wananchi hao wasijichukulie sheria mkononi kwa kumhukumu kifo kibaka huyo.

Wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com walisema kuwa kijana huyo ambaye anafahamika kwa jina la moja la Mtega ni mkazi wa eneo hilo la Kihesa na juzi alipata kuiba simu na baada ya kuipiga namba hiyo ya simu iliyoibiwa ndipo mtuhumiwa huyo alipokea na kuwekewa mtego wa kuitwa eneo la Miyomboni ambako baada ya kufika alikamatwa na kupelekwa Kihesa kwa ajili ya kuchomwa moto.

Alisema John kalinga kuwa kikundi cha vijana zaidi ya 100 na wananchi wengine wa eneo hilo walijikusanya na kutaka kutoa hukumu ya kifo kwa kijana huyo ikiwa ni pamoja na kumcharanga mapanga usoni kabla ya kutaka kumuua kwa kumchoma moto.

Alisema wakati mkakati wa kumchoma moto kijana huyo ukiandaliwa ndipo askari kanzu mmoja anayeishi katika eneo hilo alifika eneo la tukio na kufanikiwa kumuokoa mtuhumiwa huyo kutoka mikononi wa vijana hao ambao tayari walitaka kumwadhibu kwa kumuua kwa madai kuwa wamechoshwa na vitendo vya kijana huyo kufanya uharifu na kurudi uraiani bila kufungwa .

Hata hivyo alisema kuwa kijana huyo anatuhumiwa kutoroka chini ya ulinzi wa polisi akiwa na pingu ya polisi na safari hii wananchi hao walitaka kumpa adhabu hiyo ya kifo.

" Tunawashukuru sana askari wa FFU ambao walifika haraka eneo la tukio na kuweza kuwatawanya wananchi hao ambao walitaka kumchoma moto kibaka huyo pamoja na askari kwa kumtetea mtuhumiwa huyo ."

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi (SACP) Michael Kamuhanda amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa sababu ya polisi kulazimika kutumia nguvu ya ziada ni baada ya wananchi hao kumshambulia kwa kichapo askari huyo pamoja na mtuhumiwa jambo ambalo bila polisi kutumia mabomu ya machozi basi usalama wa askari wake na mtuhumiwa huyo ungekuwa hatarini.

Kamanda Kamuhanda alisema polisi wa FFU walilazimika kupiga juu mabomu mawili ya machozi kwa ajili ya kuwatawanya wananchi hao wanaojita kuwa nahasira kali na kufanikiwa kumfikisha mtuhumiwa polisi .

Hata hivyo kamanda huyo aliwaonya wananchi kuacha kuchukua sheria mkononi dhidi ya waharifu na kuwaomba kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kuwakamata watuhumiwa salama na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.
Chanzo:DJ SEK BLOG

0 comments: