Subscribe:

search

.

Thursday 23 August 2012

NAIBU WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA HAILEMARIAN DESALEGN KUSHIKIRIA WADHIFA WA ALIYEKUWA WAZIRI MKUU MPAKA HAPO UCHAGUZI UTAKAPOFANYIKA


 
Mwili wa Wariri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi  umelakiwa na maelfu  ya  watu  waliokuwa  wakilia   wakati  wa kipindi rasmi  cha   maombolezo  kikianza  baada  ya  kifo  cha  kiongozi huyo  katika  hospitali   mjini  Brussels.
Bendi  ya  jeshi  ilipiga nyimbo  za  maombolezo  wakati  jeneza , lililofunikwa  bendera  ya taifa , likitolewa  kutoka  katika  ndege  ya  shirika  la  ndege  la Ethiopia  tukio  ambalo  pia  lilihudhuriwa  na viongozi  wa  kisiasa , kidini  na  jeshi pamoja  na  wanadiplomasia.
Naibu  waziri  mkuu Hailemariam Desalegn, mwenye  umri  wa  miaka 47, ambaye  pia  ni  waziri  wa  Mambo  ya  Nje  tangu  mwaka 2010, ataongoza nchi hiyo kwa muda.
 Vyombo  vya  habari  vya  taifa  vimeripoti kuwa  kiongozi huyo atabakia  madarakani  hadi  uchaguzi  wa  mwaka  2015, licha ya  kuwa huenda  baadaye  mwaka  huu.
Meles Zenewi  amefariki  usiku  wa  Jumatatu  kuamkia  Jumanne  kufuatia kuugua  kwa  muda  mrefu.
This Day Magazine

0 comments: