Subscribe:

search

.

Thursday 23 August 2012

TASWIRA YA OPERESHENI SANGARA MVOMERO



Katibu Mkuu wa BAVICHA Deogratias Munishi akimkabidhi kadi ya CHADEMA aliyekuwa mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Kododo jimbo la Mvomero, bwana Charles Kiwaga. Wengine ni wanachama wapya wa CHADEMA tawi la Kododo Mvomero.
Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM kata ya Muhonda akieleza jinsi alivyokunwa na sera za CHADEMA zilizoelezwa na katibu Mkuu wa BAVICHA katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kichangani.

Mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Kododo, Charles Kiwaga (kulia) akifafanua kero ya shule ya msingi kododo kwa kayibu mkuu wa Bavicha Deogratias Munishi. Katikati ni mjumbe wa kamati ya maendeleo ya elimu ya shule hiyo. Shule hii ina wanafunzi 652 na mwalimu mmoja tu.

Na Mdau Hellen-Morogoro
Operesheni Sangara inayoendelea kwa upande wa Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), Bwana Deogratias Munishi amezidi naye kupasua vijiji ndani ya Mvomero, Morogoro. Pia wanavijiji walimuonyesha hali halisi ya maendeleo katika kata yao ya Luale kwa kipindi kirefu walichokuwa chini ya CCM tangu miaka 50 iliyopita mpaka sasa na wakiwa wamekata shauri kujiunga na CHADEMA kama chachu ya mabadiliko.
Chanzo:Mjengwa blog.com

0 comments: