Subscribe:

search

.

Friday 17 August 2012

PINDA AWEKA JIWE LA MSINGI DODOMA

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiweka wa jiwe la msingi katika jengo la Ofisi ya Taifa ya  Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mjini Dodoma jana. Jengo hilo jipya lenye urefu wa ghorofa nane,  linatarajiwa kuwa Makao Makuu ya Ofisi hiyo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda , akipata maelezo  kutoka kwa Meneja Ujenzi  wa jengo hilo, Casmil Muscbi. Kushoto ni  Mkuu  wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Rehema Nchimbi,  watatu  kutoka kushoto ni  Mwakilishi wa Mdhibiti  na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Athanas Pius .
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, wakati alipowasili kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika Jengo hilo jana
 Mkuu  wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Rehema Nchimbi, akishiriki kusebeneka na wasanii wa ngoma za asili, wakati wa hafla hiyo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuweka wa jiwe la msingi katika jengo la Ofisi ya Taifa ya  Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mjini Dodoma litakalokuwa na urefu wa ghorofa nane na linatarajiwa kuwa Makao Makuu ya Ofisi hiyo.Picha zote na Magreth Kinabo- Maelezo

0 comments: