search

.

Tuesday, 14 August 2012

RAY TUNAUZA HAKI ZETU KWA SABABU HATUNA JINSI.

 

Vincent Kigosi.
Ray The Greatest Mtayarishaji na muongozaji wa filamu Swahiliwood.
MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood Vincent Kigosi ‘Ray the greatest’ amefunguka kwa kusema ni kweli wasanii wanauza haki zao za filamu wanazotengeneza kwa wasambazaji kutokana na hali halisi ya soko lenyewe
kuwa finyu likimilikiwa na kampuni moja tu, ambayo angalau imewatoa hapo walipo tofauti na siku za nyuma
walivyoanza kuigiza katika televisheni.

Vincent Kigosi
Ray mtayarishaji wa filamu Swahiliwood.
Vincent Kigosi
Ray The greatest akiwa makini katika kufikiria jambo.
“Ukweli si kama tunapenda kuuza haki zetu kwa wasambazaji au wanaonunua filamu, sababu kubwa ni ukosefu wa soko la uhakika pamoja na wawekezaji kushindwa kujitokeza, lakini tuwe wakweli na kukumbuka tulikotoka tulikuwa tunaigiza katika Televisheni kwa kulipwa 40,000/ tu kundi la wasanii kibao, lakini leo hii tunamiliki kampuni na kumudu maisha yetu kwa kununua magari na vitu vingine,”anasema Ray.
Ray anasema kuwa ni jukumu la serikali kuandaa mazingira yatayoweza kushawishi wawekezaji au wadau wanaoweza kuingia katika usambazaji wa filamu, lakini jambo lingine ni taasisi za kibenki kuwadhamini kwa kuwakopesha fedha kwa ajili ya kutengenezea filamu na kuingia sokoni au kuuza hata nje ya nchi, hilo ndilo linaweza kuleta maslahi na kuwafanya wasanii wasiuze haki zao.
Chanzo:www.filamucentre.co.tz

0 comments: