search

.

Friday, 17 August 2012

TUME YA KATIBA KAZINI

 Katibu wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Neville Meena akichangia hoja wakati wa mkutano wa
kubadilishana mawazo baina ya Uongozi wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Baraza la Habari Tanzania
(MCT) pamoja na Jukwaa la Wahariri uliofanyika leo jumanne tarehe 14.Agosti.2012 Jijini Dar es Salaam.
Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph
Warioba, Katibu wa Tume Assaa Rashid na Naibu Katibu Casmir Kyuki
 Watoto hawa Saada Yusuph (7) kushoto na mwenzake Joseph Makwate (8) wa kata ya
Nzunguni Manispaa ya Dodoma mjini wakisoma nakala za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
wakati walipotembelea banda la Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika sherehe ya siku ya Wakulima
Nanenane zilizofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Nzunguni mjini Dodoma.
 Wakazi wa Manispaa ya Mji wa Dodoma wakiwa katika foleni kusubiri kuingia katika
Banda la Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati wa kilele cha siku ya Wakulima (Nanenane) zilizofanyika
hivi karibuni katika viwanja vya Nzunguni mjini humo.
IMG 5232 Bi Joyce Kasambala (70) mkazi wa Mpwapwa mkoani Dodoma akisoma machapisho
mbalimbali yanayotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati wa sherehe za Siku ya Wakulima
Nanenane zilizofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Nzunguni mjini Dodoma.

PICHA NA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

0 comments: