Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh.Magesa Mulongo akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Jeshi la Polisi wa Mkoa huu mara baada ya kuwasili katika kiwanja cha michezo kilichopo katika moja ya kambi zilizopo mkoani humo, kulia kwake ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha (ACP) Liberatus Sabas akimtambulisha viongozi hao.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Magesa Mulongo akikagua gwaride lililoandaliwa na jeshi la Polisi mkoani humowakati wa hafla ya makabidhiano ya vyeti kwa askari 37 wa mkoa huu waliofanya vizuri zaidi katika utendaji wao wa kazi za kila siku. Hafla hiyo ilifanyika tarehe 08/10/2012 katika kiwanja cha michezo kilichopo katika moja ya kambi ya jeshi hilo iliyopo Mjini Arusha.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha (ACP) Liberatus Sabas akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Magesa Mulongo ili aweze kutoa vyeti na fedha taslimu Tsh laki moja kwa kila askari ambaye alikuwa amefanya vizuri zaidi katika utendaji wake wa kazi za kila siku.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Magesa Stanslaus Mulongo akimkabidhi cheti cha utendaji bora wa kazi askari wa jeshi la Polisi mkoani humo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Jane Warioba wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika kiwanja cha michezo kilichopo katika kambi ya polisi ya Mjini Arusha tarehe 08/10/2012.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Magesa Mulongo akitoa pongezi kwa askari wote wa Jeshi la Polisi mkoani humo kutokana na utendaji mzuri wa kazi zao za kila siku katika hafla ya kuwatunuku askari 37 wa jeshi hilo mkoani hapa ambao walifanya vizuri zaidi iliyofanyika katika kiwanja cha michezo kilichopo katika moja ya kambi zilizopo mjini hapa tarehe 08/10/2012.
Baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi mkoani A warushakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kunukiwa vyeti na fedha taslimu Tsh laki moja kila mmoja kutokana na utendaji mzuri wa kazi zao za kila siku.