search

.

Tuesday, 9 October 2012

BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI LAANZA KAZI

 
Bunge la Afrika liliundwa mwaka 2004 sambamba na kuasisiwa Umoja wa Afrika AU na linahesabiwa kuwa ni miongoni mwa nguzo muhimu za umoja huo. Lengo la kuundwa bunge hilo ni kutoa fursa kwa wawakilishi wa nchi zote wanachama kukutana na kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali na kutoa ushauri kwa nchi za Afrika.
 
Bunge la Afrika lina wajumbe 265 ambao huchaguliwa na mabunge ya nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. Hata hivyo Bunge hilo la Afrika halina nguvu za kutunga sheria bali kazi yake ni kutoa ushauri tu.
Rais Boni Yayi wa Benin ambaye nchi yake ndiye mwenyekiti wa hivi sasa wa Umoja wa Afrika ameahidi kuunga mkono juhudi za kuliimarisha zaidi Bunge la Afrika.
 
Alisema jana usiku wakati wa kuanza kazi rasmi bunge hilo huko Johannesburg, Afrika Kusini, kwamba, nchi zote za Afrika zinapaswa kuunga mkono jitihada za kulifikisha bunge hilo katika kiwango cha juu cha hadhi ya bara la Afrika.

0 comments: