search

.

Tuesday, 16 October 2012

CCM YAAPA KURUDISHA MAJIMBO MANYARA

CCM mkoani Manyara kimemaliza uchaguzi wake mkuu ngazi ya mkoa, kikiadhimia kukomboa jimbo moja la uchaguzi la Mbulu na kata 34 zilizochukuliwa na vyama vya upinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Azimiohilolilitolewa na viongozi wapya waliochaguliwa wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM mkoa Lukas ole Mukusi
Mkoa wa Manyara una kata 123 na majimbo ya uchaguzi sita katika wilaya tano za mkoa huu.
Katika uchaguzi wa mwaka 2010 jimbo moja la Mbulu lilichukuliwa na CHADEMA na kata 34 zikachukuliwa na vyama vingine vya upinzani kikiwemo NCCR Mageuzi.
Uchaguzi mkuu wa CCM ngazi ya mkoa uliomalizika, viongozi waliochaguliwa wameapa kurudisha jimbo la Mbulu na kata zote 34 zilizonyakuliwa na wapinzani.
Msimamizi wa uchaguzi huo spika wa baraza la wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa Pandu Amir Kificho aliwasisitiza viongozi waliochagulia kutambua wajibu wao kwa wananchi na si maslahi binafsi.
Uchaguzi mkuu wa CCM ngazi ya mkoa mkoani Manyara, mbali na kumchagua mwenyekiti pia zimechaguliwa kamati mbili za halmashauri kuu na kamati ya siasa na uchumi ya mkoa.

0 comments: