Subscribe:

search

.

Saturday 13 October 2012

EBOLA KIKWAZO KWA WAISLAM UGANDA


Waislamu nchini Uganda mwaka huu hawatoweza kuhudhuria ibada ya kwenda kuhiji Makka baada ya utaratibu wa kuwapatia Visa kucheleweshwa kwa kuhofia ugonjwa hatari wa Ebola.
Akizungumzia suala hilo Balozi wa Saudi Arabia amesema kuwa kufikia Oktoba 4 wakati Shirika la Afya Duniani linatangaza Uganda kuwa huru dhidi ya ugonjwa huo, ilikuwa umebakia muda wa siku 5 tu kukamisha zoezi la kushughulikia mahujaji wa kigeni, muda ambao usingetosha kutoa viza kwa mahujaji wa Uganda.

 Balozi Jamal Abdul Aziz Raffa amesema japokuwa mahujaji wa Uganda hawakufanikiwa kwenda kuhiji,  lakini bado wanastahili kuitwa Hajjs na Hajjats kwa sababu walikwisha jiandaa kufanya hijja hiyo.

Ameongeza kuwa Ubalozi huo umesitisha pia kutoa viza kwa wafanyabiashara wa Uganda wanaotaka kuelekea Saudi Arabia mpaka hapo watakapojiridhisha kuwa sasa hali ni shwari.
Jumla ya mahujaji 900 walikuwa wamejiandikisha kwa safari ya Makka mwaka huu.
Hii ni mara ya pili katika kipindi cha miaka 12 mahujaji wa Uganda wanashindwa kwenda Saudi Arabia kuhiji kutokana na tatizo la Ebola.

Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2001 wakati ugonjwa huo hatari ulipoikumba wilaya ya Gulu.

0 comments: