Subscribe:

search

.

Saturday 13 October 2012

WAANDISHI 16 WAMEUAWA SOMALIA 2012

 Waandishi wa habari kumi na sita wameuliwa hadi sasa mwaka huu kwa mabomu na watu wenye silaha, jambo linalothibitisha kwa nini watetezi wa haki za vyombo vya habari, Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka (RSF) wameuita mwaka 2012 kuwa "mwaka wa vifo" katika kumbukumbu za waandishi wa habari wa Somalia, kupita mwaka 2009 ambapo waandishi tisa walifariki.

 RSF waliita nchi hivyo baada ya mabomu mawili ya kujitoa muhanga kuua kiasi cha watu 14, ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari watatu hapo tarehe 20 Septemba. Wiki moja baadaye, waandishi wa habari wawili zaidi waliuliwa katika mji mkuu.
Wasimamizi wa Haki za Binadamu (HRW) waliitaka serikali mpya ya Somalia kuagiza ufanyike uchunguzi katika mauaji ya waandishi wa habari.

"Waandishi wa habari wa Somalia wamekuwa kwa muda mrefu wa mwanzo katika orodha ya walengwa wa pande zote wakati wa vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe," Leslie Lefkow, naibu mkurugenzi wa HRW sehemu ya Afrika, alisema hapo tarehe 24 Sepetemba. "Rais mpya wa Somalia anaweza kuchukua hatua za kumaliza mtindo huu wa kutisha kwa kuagiza kufanyika uchunguzi wa haraka na makini kuhusu mauaji haya."

Hii sio mara ya kwanza kwa RSF kutoa tahadhari juu ya vurugu dhidi ya waandishi wa habari nchini Somalia. Mwaka 2011, waliita Somalia kuwa ni taifa la vifo vingi zaidi vya waandishi wa habari barani Afrika, na kuongeza kuwa tayari waandishi wa habari 25 waliuawa nchini Somalia kuanzia mwaka 2007 hadi 2011.
Tarehe 28 Januari: Watu wenye bunduki wasiojulikana walimpiga risasi na kumuua Hassan Osman Abdi, aliyekuwa anajulikana kama Hassan Fantastic, karibu na makazi yake kenye wilaya ya Wadajir, kusini ya Mogadishu. Alikuwa mkurugenzi wa Mtandao huru wa habari, Shabelle Media Network. Rais wa wakati ule Sharif Sheikh Ahmed alipendekeza kuwa al-Shabaab walihusika na kifo cha Abdi.
Tarehe 28 Februari: Watu wenye bunduki wasiojulikana walimpiga risasi na kumuua Abukar Hassan Kadaf, aliyekuwa mkurugenzi wa Redio Somaliweyn, nje ya nyumba yake mjini Mogadishu.
Tarehe 4 Machi: Mwandishi wa habari Ali Ahmed Abdi alipigwa risasi na kuuawa kaskazini ya mkoa wa Galkayo wakati akielekea nyumbani kutoka kazini kwake huko Redio Galkayo.
Tarehe 5 Aprili: Mshambulizi asiyejulikana alimpiga risasi na kumuuua Mahad Salad Adan huko Beledweyne, mkurugenzi wa Voice of Hiran, kituo cha redio cha eneo na ripota wa Redio Shabelle ya Mogadishu. Aliripoti juu ya migongano baina al-Shabaab na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali Ahlu Sunna wal Jamaa.

Tarehe 3 Mei: Watu wenye silaha waliojifunika nyuso walimpiga risasi na kumuua Farhan Jeemis Abdulle, ripota wa Redio Daljir huko Galkayo, wakati alikuwa akielekea nyumbani.
Tarehe 24 Mei: Wavamizi wasiojulikana walimpiga risasi Ahmed Addow Anshur wa Shabelle Media Network karibu na nyumba yake kwenye wilaya ya Dharkenley mjini Mogadishu.
Tarehe 7 Julai: Abdikadir Omar Abdulle, mwandishi wa habari katika Universal TV inayomilikiwa binafsi, alipigwa risasi mara nne na watu wenye silaha wasiojulikana karibu na nyumbani kwake katika wilaya ya Madina ya Mogadishu, lakini alinusurika kifo.
 Tarehe 31 Julai: Somali journalist and comedian Abdi Maleq Jeylani, aliyekuwa akijulikana kama Marshale, alipigwa risasi na kufa nje ya nyumba yake katika wilaya ya Waberi mjini Mogadishu. Jeylani alifanya kazi katika vituo kadhaa vya redio na televisheni, huku akishiriki katika kuwakosoa al-Shabaab.
Tarehe 12 Agosti: Mwandishi wa habari mkongwe na meneja wa mahusiano ya vyombo vya habari katika Wizara ya Habari, Simu na Mawasiliano Yusuf Ali Osman alipigwa risasi na mtu asiyejulikana katika wilaya ya Dharkenley.
 Mwandishi wa habari wa Redio Sauti ya Demokrasia Mohamud Beneyste, akiwa na umri wa miaka 22, aliuliwa jioni siku hiyo wakati akipiga picha karibu na uwanja wa Michezo wa Mogadishu.
Tarehe 16 Septemba: Watu wasiojulikana wenye silaha walimuua mpiga picha wa kujitegemea Zakariye Mohamed Mohamud Moallim mjini Mogadishu.
Tarehe 20 Septemba: Mabomu mawili ya kujitoa muhanga yaliua kiasi cha watu 14 na kujeruhi wengine 20 katika mkahawa mjini Mogadishu. Waandishi wa habari watatu waliuliwa katika shambulio hilo: Liban Ali Nur, mkuu wa idara ya habari katika Televisheni ya Taifa ya Somalia; Abdisatar Dahir Sabriye, mkuu wa uandaaji vipindi katika Televisheni ya Taifa ya Somalia; na Abdirahman Yasin, mkurugenzi wa kituo huru cha redio Sauti ya Demokrasia.
Mwandishi wa habari wa nne, Hassan Yusuf Absuge wa Redio Maanta ambayo ni redio huru, alipigwa risasi hatimaye na kufariki baada ya kufanyia kazi ripoti kuhusu shambulio hilo la kujitoa muhanga.
Tarehe 27th: Septemba: Mwili uliokatwaa kichwa wa mwandishi wa habari wa michezo Abdirahman Mohamed Ali uligunduliwa katika wilaya ya Huriwa ya Mogadishu. Ali alikuwa ametekwa nyara na watu waliokuwa na silaha kutoka nyumba moja karibu na Meat Market mapema siku hiyo. Alikuwa anafanyia kazi mtandao wa habari Ciyaaraha Maanta.
Tarehe 28th: Septemba: Watu wasiojulikana wenye silaha walimpiga risasi na kumuua Ahmed Abdulahi Fanah, mwenye umri wa miaka 32 mwandishi wa habari anayefanyia kazi shirika moja la habari la Yemeni, katika wilaya ya Dharkenley.

0 comments: