search

.

Tuesday, 16 October 2012

KUNAWA MIKONO KUTAEPUSHA VIFO VYA WATOTO


Wakati dunia inaadhimisha mwaka wa tano wa kimataifa wa kunawa mikono kwa sabuni, Shirika la kuhudumia watoto duniani, UNICEF limesema kitendo hicho kinaweza kuokoa maisha ya maelfu ya watoto wanaokufa kila mwaka.

Takwimu za mwezi uliopita za UNICEF kuhusu vifo vya watoto zinaonyesha kuwa watoto Elfu Mbili wenye umri wa chini ya miaka mitano walikufa kila siku kutokana na magonjwa ya kuhara yanayotokana na uchafu na uhaba wa maji safi na salama.

Mshauri mwandamizi wa UNICEF kuhusu usafi Therese Dooley ameema magonjwa ya kuhara kimsingi yanatokana na kula kinyesi na hivyo ni vyema kunawa mikono kwa sabuni kabla ya kula chakula, baada ya kujisaidia na hata baada ya kumbadilisha mtoto nepi.
Bi. Dooley amesema wanataka watoto, familia, jamii na mataifa kufahamu kuwa kitendo cha kudhibiti kusambaa kwa magonjwa ya kuhara siyo kigumu, siyo cha gharama na kwamba kunawa mikono kwa sabuni ni lazima kiwe kitendo cha kila siku.

UNICEF ilifanya utafiti na kubaini kuwa tabia ya kunawa mikono kwa sabuni inatofautiana kutoka nchi hadi nchi kulingana na makazi, utamaduni na hali ya kiuchumi.

0 comments: