search

.

Tuesday, 16 October 2012

CANNAVARO : SIMBA WAJIANDAE TUMESHAFIKA


Nahodha wa kikosi cha  mabingwa wa  soka afrika Mashariki na kati  Yanga , Nadir Haroub Cannavaro(pichani kulia) ametoa onyo kwa  watani wa jadi wa  timu hiyo Simba  Sport Club  wajiandae kuachia kiti cha  uongozi wa ligi kuu ya Vodacom wanachokikalia hivi sasa .

Akizungumza na HABARITANZANIA mapema leo Cannavaro amesema kuwa  pengo la pointi sinta lililopo baina ya timu hizo mbili siyo kubwa na Yanga ina uwezo wa kulifikia na kuvuka wakati wowote.
“Tuna pengo la pointi sita  dhidi ya watani zetu, ninachotaka kuwaambia ni kuwa wajiandae tu kutupisha kwenye kiti cha  uongozi kwani  hizo ni pointi chache ambazo tunazifikia wakati wowote  na kuzivuka kwani sasa yale matatizo yaliyokuwa yanaikabili timu yetu yameshawekwa sawa kilichpo sasa ni kushinda kila  mchezo unokuja mbele yetu” alisema Cannavaro

Katika hatua nyingine Cannavaro amesema kuwa  hali ya beki kisiki katika kikosi hicho Kelvin Yondani inaendelea vizuri na wakati wowote ataanza kukipiga kwenye michezo inayokuja ya ligi kuu ya Vodacom

0 comments: