search

.

Monday, 8 October 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHITIMISHA MATEMBEZI YA HISANI
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki katika matembezi ya hisani ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga uwezo wa Wahandisi wa Tanzania, yaliyoandaliwa na Wahandisi hao (Local Engineers). Matembezi hayo yalianzia katika Viwanja vya Karimjee jijini na kumalizikia katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki mazoezi ya viungo baada ya kumaliza kushiriki na kuhitimisha matembezi ya hisani ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga uwezo wa Wahandisi wa Tanzania, yaliyoandaliwa na Wahandisi hao (Local Engineers). Matembezi hayo yalianzia katika Viwanja vya Karimjee jijini na kumalizikia katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Moahammed Gharib Bilal,akimkabidhi cheti, Mhandisi Grace Beo, kutoka Kampuni ya Temesa ICT Engineer, akiwa ni mmoja kati ya waliochangia na kushiriki vyema katika zoezi la kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga uwezo wa Wahandisi wa Tanzania, yaliyoandaliwa na Wahandisi hao (Local Engineers). Makamu alikabidhi vyeti hivyo baada ya kuhitimisha rasmi matembezi hayo ya hisani yaliyoanzia katika Viwanja vya Karimjee na kumalizikia kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Moahammed Gharib Bilal,akimkabidhi cheti, Mhandisi Morgan Nyonyi,  kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), akiwa ni mmoja kati ya waliochangia na kushiriki vyema katika zoezi la kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga uwezo wa Wahandisi wa Tanzania, yaliyoandaliwa na Wahandisi hao (Local Engineers). Makamu alikabidhi vyeti hivyo baada ya kuhitimisha rasmi matembezi hayo ya hisani yaliyoanzia katika Viwanja vya Karimjee na kumalizikia kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na Wahandisi (Local Engineers) baada ya kuhitimisha matembezi hayo katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Daar es Salaam.

0 comments: