search

.

Tuesday, 16 October 2012

MBIO ZA KUWANIA URAISI KENYA ZAENDELEA

Wanasiasa waliendelea na kampeni zao hii leo, huku chama cha ODM kikiendelea na kampeini zake katika eneo la Dandora, ambako Waziri Mkuu Raila Odinga aliongoza mikutano hiyo. Mbunge wa Eldoret Kaskazini William Ruto alikuwa eneo la Mombasa alikoendeleza kampeini zake, naye Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka akiwa katika eneo la Machakos, aliposema kuwa bado ni mshikadau katika muungano wa G7, ila hawajaafikiana ni nani atakayepeperusha bendera katika uchaguzi mkuu.

0 comments: